Japo utajiri huo hauwanufaishi wananchi wengi wa nchi hiyo lakini bado inabaki kuwa ni mojawapo ya nchi tajiri Afrika
Pamoja na utajiri huo nchi hiyo pia watu wake wengi ni wasomi na wenye kupenda kujifunza mambo mapya
Kwa upande wa imani ni hakika kuwa kwa sasa kwa afrika ni nchi yenye wahubiri wengi na wakubwa wa dini ya Kikristo.Wahubiri hao sio tu wakubwa na wenye kuheshimika pia ni wenye mafanikio mengi zaidi ya mali na kuwa na mahekalu makubwa yenye kuchukua watu wengi zaidi kwa wakati mmoja
Utajiri wao (tofauti na wachungaji wengine) unatokana na shughuli na kazi mbalimbali wanazozifanya kama vile shule, vyuo, mashamba nk, na hawategemei sadaka kama wafanyavyo wahubiri wengi wakiwepo baadhi waliopo nchini kwetu
Ifuatayo ni orodha ya wahubiri (pastors) wenye utajiri mwingi zaidi nchini Nigeria
1. - Bishop David Oyedepo
Huduma yake inaitwa - Living Faith Worls Outreach Ministry aka Winners Chapel
Utajiri wake unakadiriwa kuwa na thamani ya $ 150 millioni
Huduma yake ilianza mwaka 1981, na kuendelea kukua mwaka hadi mwaka.Hua anakua na huduma ya ibada tatu kwa siku za jumapili, ni huduma kubwa zaidi Afrika.Kanisa lake linaweza kuchukua waumini 50,000.Oyedepo anamiliki ndege aina ya jeti 4 na ana nyumba za kisasa katika jiji la London na Marekani. Pia ana kiwanda cha uchapaji, , ana chuo kikuu kinachoitwa Covenant University, na shule nyingi nchini Nigeria
2. Chris Oyakhilome
Huduma yake inaitwa Believers Lovewold Ministries a.k.a Chris Embassy
Utajiri wake unakadiriwa kuwa na thamani ya $ 30 milioni - $ 50 milioni
Kanisa lake linakadiriiwa kuchukua waumini mpaka 40,000 kwa wakati mmoja wengi wao wakiwa ni wafanyabiashara na wanasiasa
Utajiri wake unatokana na kuwa na vyombo vya habari kama magazeti, television, studio ya kurekodi, hoteli na majumba mbalimbali.
3. Temitope Joshua (TB Joshua)
3. Temitope Joshua (TB Joshua)
Huduma yake inaitwa Synagogue church of all Nations (SCOAN)
Utajiri wake unakadiriwa kuwa na thamani ya $ 10 milioni - $15 milioni
Huduma yake ilianza mwaka 1987, ambapo huduma yake inachukua watu 15,000 siku za jumapili.
Mtumishi huyo anafanya huduma ya uponyaji kama wa kansa, ukimwi na hata kuponya wagonjwa wa kupooza kwa mafanikio makubwa
Huduma hii imekua na kuenea katika nchi za Ghana, Uingereza, Afrika Kusini na Ugiriki.
Anamiliki Emmanuel Tv ambayo ni televisheni ya kikristo na ni rafiki mkubwa wa Rais wa Ghana Atta Mills
4.Mathew Ashimolowo
Huduma yake inaitwa Kingsway International Christian Center (KICC)
Utajiri wake unakadiriwa kuwa na thamani ya $6 millioni - $10 millioni
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali alizo nazo kama vile vyombo vya habari kama magazeti, na televisheni
5.Chris Okotie
Huduma yake inaitwa Household of God Church
Utajiri wake unakadiriwa kuwa na thamani ya $3 milioni - $10 milioni
Huduma yake hii ina waumini wapatao 5,000 ambapo wengi ni waigizaji wa Nollywood , wanamuziki na watu wengine wa kawaida.
Amewahi kugombea uraisi kwa chama cha Fresh Party mara tatu lakini hajawahi kupata.
Anamiliki Mercedes S600, Hummer na gari aina ya Porshe mbali na magari mengine mengi ya kifaharia anayomiliki