Latest News


More

SAMSON APATA KIPAIMARA

Posted by : Unknown on : Friday, December 28, 2012 0 comments
Unknown

Samson Wande Kichila alipata kipaimara mwishoni tarehe 16/12/2012 huko nyumbani kwa wazazi wao Mkokozi - Kongowe
Ibada ya Kipaimara ilifanyika kwenye kanisa la K.K.KT  mtaa wa Mkokozi lililoko maeneo hayo ya nyumbani kwao  na kuhudhuriwa na ndugu jamaa  marafiki  na majirani wa karibu.
Kipaimara ni hatua muhimu kwa wakristo wa K.K.K.T kwani ndio hatua ya mkristo kukiri kwa kinywa cheke kumpokea Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wa maisha yake
 Pichani juu  ni viongozi wa kanisa walioendesha ibada hiyo.Mchungaji wa Usharika wa Kurasini (ambao ndio walezi wa Mtaa huo na mwinjilisti wa mtaa huo wa Mkokozi
 Picha za Juu Samson (aliyeshika cheti) baada ya kupata kipaimara akiwa na baadhi ya ndugu na jamaa kwa picha ya pamoja
 Samson akiwa na mpambe wake Noel Range na mpambe mdogo Richard Samwel

 Baadhi ya ndugu na jamaa na marafiki wakiwa ukumbini kwenye sherehe ya kumpongeza Samson kwa kupata Kipaimara
 Blog hii innamtakia kila la heri Samson katika safari yake ya Kiroho

No comments:

Leave a Reply