Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji Kiongozi Mchungaji Kaanasia Msangi akisaidiana na Parish Worker wa Usharika huo
Katika mahubiri yake mchungaji huyo alisisitiza Upendo kwa waumini wote na pia kujiepusha na vitendo viovu ili kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuwe na maana katika maisha yao ya Kiroho
Kwaya mbalimbali zilihudumu katika ibada hiyo kama kwaya ya Uinjilisti, Kwaya Kuu na kwaya ya watoto wa jumapili (Sunday School).Pichani juu watoto wa shule ya jumapili wakionyesha ngonjera iliyowasisimua sana waumini
Watoto wa shule ya jumapili wakiimba ngonjera kwa hisia kali
Waumini mbalimbali wakifuatilia ngonjera ya watoto.Aliyevaa suti nyeusi ni mwinjilisti wa usharika Mwinjilisti Shayo
Picha ya juu na chini baadhi ya waumini wakifuatilia ibada hiyo
Watoto wa shule ya jumapili wakiendelea na ngonjera yao kanisani Mwenge
Pichani juu na chini watoto wa shule ya jumapili wakifuatilia ibada hiyo
Mama Evelyn na Evelyn nao walikua kwenye ibada hiyo ya Krismas
Hawa nao badala ya kusali waliendelea na ibada yao nje ambao haikuwa na mchungaji wala kiongozi.Hakika utoto ni mzuri sana
No comments: