Latest News


More

IBADA YA UZINDUZI WA KWAYA YA K.K.K.T.USHARIKA WA NKUHUNGU (DODOMA)

Posted by : Unknown on : Tuesday, April 23, 2013 0 comments
Unknown
Jumapili ilifanyika ibada ya baraka kubwa katika Usharika wa K.K.K.T Nkuhungu Dodoma.Pamoja na ibada hiyo kulikua na tendo la uzinduzi wa album ya kwaya ya Usharika huo.Album hiyo yenye jina la YAINUE MACHO, ni ya kwanza kwa kwaya hiyo ya Usharika.Mgeni rasmi kwenye uzindizi huo alikua ni naibu waziri wa ujenzi Mheshimiwa Greyson Lwenge.
 Washarika wakiwa katika ibada ya uzinduzi huo katika Usharika wa K.K.K.T Nkuhungu - Dodoma.Mbele aliyesimama ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mheshimiwa Greyson Lwenge (naibu waziri wa Ujenzi)


 Msaidizi wa askofu wa Dayosisi ya Dodoma (K.K.K.T) Mchungaji Samweli Mshana akimkabidhi DVD naibu waziri wa Ujenzi Mh.Greyson Lwenge kwa ajili ya uzinduzi wa album yao ya kwanza.
 Mheshimiwa Naibu waziri Grayson Lwenge akikabidhi mmoja wa washarika Bwana Makundi mojawapo ya CD aliyoinadi.Kushoto ni Bwana Baraka Maimu mmoja  wa wanakwaya akifuatiliwa na Ndugu George Urio ambaye alikua mmojawapo wa washereheshaji wa uzinduzi huo.
 Kwaya ya watoto ya Compassion TGC-K.K.K.T Usharika wa Nkuhungu - Dodoma wakiwasindikiza kwaya ya Usharika kwa ajili ya uzinduzi wa album yao ya kwanza.
 Baadhi ya wanakwaya wa Usharika wa Nkuhungu wakiwa kwenye ibada ya uzinduzi kanisani kwao Nkuhungu - Dodoma
 Mc Ely Msuya akiwa tayari kwa ajili ya kunadisha DVD ya kwaya ya Usharika wa Nkuhungu - K.K.K.T DODOMA
Wanakwaya wa kwaya ya Usharika wa Nkuhungu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa album yao ya kwanza.Hakika Yesu ni Bwana , walisikika wakisema wanakwaya hao kwani bwana Mungu aliwapigania na kuwawezesha kufanya uzinduzi salama wa album yao ya kwanza
Matarajio yao ilikua kukusanya shilingi milioni 12, lakini zilipatikana milioni takriban 8 ambazo ni ahadi pamoja na fedha taslimu
Wanatarajia kutumia fedha hizo kununulia vyombo vya muziki vya kisasa kwa ajili ya kwaya yao.

Sifa na Utukufu kwa Bwana!!

Picha na taarifa kwa hisani ya Ely Msuya (Dodoma)

No comments:

Leave a Reply