Ibada hiyoiliyokuwa na waumini wengi ilihudhuriwa pia na viongozi takribani wote wa Dayosisi hiyo na wachungaji wa sharika mbalimbali ilitanguliwa na maandamano ya wanakwaya na wachungaji wakiongozwa na kwaya ya matarumbeta ya Usharika wa Wazo Hill
Picha ya juu Mgeni rasmi Askofu Dr.Alex Gerhaz Malasusa akiwa kwenye maandamano tayari kwenda kuweka jiwe la msingi la kanisa hilo.Aliyeongozana naye pembeni ni mchungaji toka Marekani
Askofu Dr Alex Gerhaz Malasusa akiongoza ibada ya kuweka jiwe la msingi.Aliyeko mbele kulia ni mchungaji kiongozi wa Usharika wa Magomeni Mchungaji Henry Mwinuka.Nyuma ya mchungaji Mwinuka ni mwenyekiti wa kamati ya ujenzi engineer Angaufoon NkyaWanakwaya wa kwaya kuu ya Msasani wakiimba katika ibada hiyo
Kwaya ya watoto wa Usharika wa Magomeni wakiimba katika ibada hiyo ya harambee
Askofu Dr Alex Gerhaz Malasusa ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akiendesha ibada.
Waumini na wageni mbalimbali wakifuatilia ibada hiyo kwa makini.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa mbele na Askofu Dr Alex Gerhaz Malasusa.Mbele kabisa ni mheshimiwa Philip Mangula (makamu mwenyekiti wa CCM Bara) akiwa na mke wake wakitoa ahadi yao.Aliyeko kushoto kwake (mwenye miwani) ni mkuu wa majeshi nchini General Davis Mwamunyange
Mke wa mchungaji toka Marekani akitoa sadaka katika ibada hiyo.Nyuma yake ni mke wa Askofu wa K.K.K.T Dr Alex Gerhaz Malasusa.Pembeni aliyesimama ni mzee wa kanisa la Usharika wa Magomeni ambaye pia alikua mwenyekiti wa kamati ya kumbukumbu ya harambee hiyo Mzee James Mushi.
Washarika na wageni mbalimbali wakiwa watulivu wakifuatilia ibada hiyo ya harambee.
Ibada hiyo ilihudhuriwa pia na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari wakiwepo wa Upendo Fm Redio ambao walikua wakirusha ibada hiyo moja kwa moja (live) kama wanavyoonekana pichani juu.
Katibu wa baraza ndugu Elius Mziray akisoma risala ya maendeleo ya ujenzi ulikofikia mpaka sasa .Ujenzi wa Nyumba hiyo ya ibada kwa mujibu wa maelezo ya katibu huyo unategemewa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 2.Mpaka sasa ujenzi umeshatumia kiasi cha shilingi milioni 500.
Katibu huyo alisema jengo hilo la kumwabudu Mungu likikamilika linatazamiwa kuchukua waumini 1800, likiwa na vyumba vya ofisi 4, vyumba vya mikutano/semina 4, vyenye uwezo wa kuchukua watu 60 hivi kila kimoja
Wanakwaya wa Magomeni wakiimba katika ibada hiyo.Wanakwaya hawa waliimba wimbo uliokuwa unahimiza watu kujenga nyumba ya Bwana.
Mkuu wa majeshi General Davis Mwamunyange akitoa ahadi yake siku hiyo ya harambee mbele ya Askofu Dr Alex Gerhaz Malasusa
Mkuu wa majeshi General Mwamunyange akiwa ameshika saa kubwa yenye picha ya kanisa jipya ambayo ilinadiwa siku hiyo ya mnada
Ulinzi uliimarishwa sana katika maeneo ya kanisa.Pichani askari wa jeshi la polisi wakiwa wanapata chakula mara baada ya kazi ya harambee kukamilika.
Mungu awabariki wote waliofanikisha harambee hiyo
No comments: