Katika ziara yake hiyo ya siku mbili ya kiserikali pamoja na mambo mengine alizungumzia kuhusu jinsi Marekani itakavyosaidia Afrika kupata umeme wa uhakika
Pichani rais Kikwete pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na balozi wa Marekani nchini Tanzania wakimpungia rais Obama mara baada ya kupanda kwenye ndege yake jana
Kabla ya kuondoka uwanjani alipata nafasi ya kuagana na viongozi mbalimbali wa serikali .Pichani akiagana na meya wa jiji la Dar es salaam huku meya wa Ilala na balozi wa Tanzania nchini Marekani balozi Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao
Awali kabla ya kuondoka Rais Obama alipata nafasi ya kupigiwa wmbo wa taifa wa nchi yake pamoja na wimbo wa taifa la Tanzania .Pichani akipokea saluti wakati zikipigwa nyimbo hizo
Kabla ya hapo rais Obama alipata nafasi asubuhi ya kukagua mitambo ya kufua umeme ya Symbion ambayo ni ya wawekezaji toka nchini Marekani.Pichani juu akitoa maneno machache wakati akiwa kwenye eneo la mitambo hiyo Ubungo
Rais Obama akionyesha ujuzi wa kucheza na mpira unaoweza kufua umemeRais Kikwete na mwenyeji wake rais Obama wakipata maelezo ya mpira unaoweza kufua umeme toka kwa mtaalam
Rais Kikwete akicheza mpira maaluma ambao unajaa nishati kila unapochezwa hivyo kutumiwa kuchajia simu au kuwasha taa kwenye eneo la mitambo ya Symbion jana
No comments: