Rais wa Marekani bwana Baraka Obama hatimae amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili.Rais huyo aliwasili mida ya saa nane na nusu mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakuu wa serikali.Rai Obama (pichani juu) aliambatana pamoja na watu wengine mke wake na mabinti zake wawili
Viongozi mbalimbali waliongozana na rais Kikwete ambao ni rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr Shein, waziri mkuu mheshimiwa Peter Pinda na viongozi wengine waandamizi wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania

Rais Obama akisalimiana na mwenyeji wake Rais Kikwete wa Tanzania mara baada ya kuwasili uwanja wa wa ndege
Rais Obama akikagua gwaride lililoandaliwa na jeshi la wananchi wa Tanzania
Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Mwamunyange akisalimiana na rais Barak Obama wa Marekani
Rais Obama akisalimiana na rais wa Zanzibar mheshimiwa Dr Shein
Rais Obama akifurahia ngoma mbalimbali ambazo zilikuwa zikitumbuiza uwanjani hapo.Pembeni ni mwenyeji wake Rais Kikwete, mke wa Rais Obama Michele na mke wa rais Kikwete mama Salma Kikwete
Rais Obama akifurahia ngoma pamoja na mwenyeji wake rais wa Tanzania mheshimiwa Kikwete mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege

Rais Kikwete na mgeni wake rais Obama wakiingia ikulu huku akilakiwa na watu mbalimbali waliofika maeneo ya ikulu kumlaki

Rais Obama akisalimiana na watu mbalimbali waliofika kumlaki katika viwanja vya ikulu mara baada ya kuwasili
Rais Obama na mwenyeji wake rais Kikwete wakiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya ikulu
Rais Obama na mwenyeji wake rais Kikwete akijiandaa kupanda mti wa ukumbusho katika maeneo ya ikulu mara baada ya kuwasili ikulu
Rais Obama akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu mara baada ya kuupanda jana katika viwanja vya ikulu
No comments: