Usharika wa Mwenge wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (K.K.K.T) umefanya siku maalum ya familia lengu likiwa ni kukutanisha wazazi na watoto ili kumwabudu Mungu kwa pamoja
Tukio hilo kubwa lilifanyika usharikani hapo likiwa limeandaliwa wamati huu ambao wanafunzi wengi wako likozo ili kuhakikisha kuwa wanasherehekea siki hiyo pamoja na wazazi wao .
Akizungumza wakati wa ibada hiyo Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi (aliyeko kwenye picha ya juu) alisema wakati huu ambao kanisa linaadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwake, kanisa linasisitiza umoja ndio maana nao wameona ni vyema kukutana na familia za Usharika huo ili kuendeleza umoja huo
Alisema kuna baadhi ya familia ambazo hufanya matembezi kwenye maeneo ambayo hayampi Mungu utukufu, hivyo imefika wakati sasa kubadilisha mtazamo na kukutana na familia kanisani ili kusherehekea kwa pamoja kwa kumsifu Mungu
Mwalimu akifundisha kwa msisitizo kundi la wanafamilia .Kundi hili lilikua linajumuisha familia ya mke na mume
Familia mbalimbali zilikiaa pamoja kama mme na mke na kupata mafundisho ya ndoa na familia
Mwalimu wa kwaya ya Vijana mwalimu Mushi akiwa kwenye semina hiyo
Dr Eliwaza akiwa na mume wake kwenye semina hiyo ya family day
Bwana Mushi na mke wake nao wakifuatilia semina hiyo kwa makini
Bwana Urio na mke wake wakifurahia semina hiyo ya neno la Mungu
Mwinjilisti Mwigune akifundisha kwenye semina hiyo
Mzee Severe na mke wake nao wakifuatilia semina hiyo
Bwana na Bi somi wakifuatilia semina hiyo
Baadhi ya wana kamati wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mchunhgaji wa Usharika huo wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi.Kutoka kushoto Mwinjilisti Mwigune, binti wa mchungaji. mchungaji Kaanasia na Mzee Godilisten Lema
Wanandoa walipata pia nafasi ya kukumbushia siku walipofunga ndoa.Hakika ilikua siku ya kukumbukwa usharikani hapo
Tukio hilo kubwa na la kihistoria liliwakutanisha wanafamilia mbalimbali wa Mwenge ambapo waliimba pamoja, kula pampja na watoto pia walipata nafasi ya kucheza pamoja
Mzee Lema Kulia (mmojawapo wa wanakamati ya maandalizi ya family day) akiwa na mwinjilisti wa Usharika Mwigune
Mzee wa kanisa mama Palangyo naye alikuwepo siku hiyo ya family day
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafamilia na wakufunzi wa semina hiyo
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi mara baada ya semina hiyo ya aina yake.
Siku hiyo kulikua na Ibada moja tu ambayo ilianza saa moja asubuhi na ilipofika saa tatu waumini walipata chai kwa pamoja kasha wakajigawa kwenye makundi mbalimbali kama vile Vijana, wajane , wagane, wazee, wanandoa wa kundi la kati, wakina mama nk.
Katika makundi hayo kulikua na waalimu waliofundisha masomo mbalimbali.Ilikofika mchana walipumzika kwa kupata chakula cha mchana kasha wakarudi tena kwa makundi tofauti na waalimu tofauti.Baada ya masomo hayo jioni walikutanika tena kwa pamoja kasha wakafanya maombi ya pamoja na kufunga sherehe hiyo , alisema ndugu Lema
No comments: