2KOR 9:6-7
Jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge imefanyika ibada nzuri .Ibada hiyo ambayo iliambatana na semina ya neon la Mungu iliyotolewa na mwalimu Edward Kawiche na kuongozwa na Mchungaji kiongozi wa Usharika Mchungaji Kaanasia Msangi akisaidiana na Mwinjislistio wa Usharika huo mwinjilisti Anna Mwigune
Katika mafundisho yake mwalimu Kawiche alikua na kichwa cha somo kinachosema “JINSI YA KUPANDA KATIKA UFALME WA MUNGU”
Mwalimu Kawiche alisema katika kupanda katika ufalme wa Mungu kuna mambo makuu yafuatayo ya kuzingatia
1.Zingatia njia na wakati sahihi wa kupanda kwani kuna wakati wa kiangazi, wakati wa masika na wakati wa vuli
2.Zingatia aina ya mbegu unayoipanda na ubora wake – kwani mavuno yako yatategemea aiana ya mbegu uliyotumia
3. Ukubwa wa shamba lako ndio unaokuwezesha kujua wingi wa mbegu utakazotumia kupanda
4.Mazingira ya shamba unalilipanda – Kama lina rutuba , kama lina magugu ni lazima uyatoe kabla ya kupanda, nk
5. Panda ukiwa na imani ya kuvuna
Ebrwania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”
- Unapoanza kupanda lazima uwe na hakika ya kwenda kuvuna
- Hagai 1:2-6
Juu na chini ni picha mbalimbali za waumini wa Usharika wa Mwenge wakifuatilia ibada hiyo siku ya jumapili
Mwalimu Kawiche alisema kuwa Kiwango cha mtu kupanda ndicho kiwango chake cha kuvuna
Vile vile katika kumtolea Mungu sadaka.Jinsi unavyotoa ndivyo hivyo hivyo utakavyovuna
Mungu hataki bora sadaka bali anataka sadaka bora
Ukitoa kidogo tarajia kupata kidogo na ukimtolea Mungu kiasi kikubwa tarajia Baraka kubwa pia
Mhu 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”
Wakati wa Bwana ukifika;chukua hatua usiangalie vikwazo vinavyokuzunguka
Mwanzo 4:1-8a
Semina hiyo ya neno la Mungu itakua inaendeshwa kila siku ya jumapili kwa muda wa mwezi mmoja na itakua inafanyika kwenye ibada zote mbili ya kwanza na ya pili
No comments: