Askari polisi wa Wilaya ya Hai
wakianda mwili wa mfanyabiashara wa madini Erasito Msuya aliyeuawa kwa kupigwa
risasi katika eneo la Wasomali, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuupeleka
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospiotali ya wilaya hiyo. Picha na Dionis
Nyato
Moshi.
Mfanyabiashara tajiri wa
Mirerani na Jijini Arusha, Erasto Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20
kwa kutumia bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), jana mchana.
Erasto anayemiliki vitega uchumi
kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani
wanaoongoza kwa utajiri,
aliuawa jana saa 7:00 mchana
wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
“Eneo la tukio kumeokotwa maganda
karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu
kwa kweli ameuawa kinyama sana,” alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomang’ombe.
Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea
kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa
Bomang’ombe, mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na
Mererani.
Habari za uhakika zilieleza kuwa
wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo,
walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya
fedha.
Kulingana na vyanzo vya habari,
mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa
Bomang’ombe na makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda
Arusha.
RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00
mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya barabara ya
Kia.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa
Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la
Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara,” alisema.
Kamanda Boaz alisema alipofika eneo
hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya
gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.
Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye
gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye
gari la Erasto
No comments: