Ibada hiyo iliongozwa na mkuu huyo wa kanisa, Msaidizi wa askofu mchungaji Fupe, Mkuu wa jimbo la Kaskazini mchungaji Anta Muro , mkuu wa jimbo la Magharibi na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi
Mkuu wa Kanisa la K.K.K.T Dr.Malasusa akiongozana na viongozi wengine wa kanisa kuingia ibadani
Akizungumza katika ibada hiyo ya harambee katibu mkuu wa Usharika wa Mwenge mzee Kombe (pichani juu) alisema ujenzi wa kanisahilo ulianza mwaka 2007 na mpaka kanisa hilo kukamilika kabisa linatazamiwa kugharimu kiasi cha shiliingi 1.2 bilioni.na litakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa wakati mmoja
Mzee Kombe alisema mpaka sasa ujenzi wa kanisa hilo umekwishafgarimu kiasi cha shilingi 533 milioni.Awamu iliyopo kwa sasa ni awamu ya tano ambayo inatazamiwa kuchukua kiasi cha shilingi milioni 360 ambao utagharimu kuweka granite (sakafu) utengenezaji wa mfumo wa umeme, uwekaji wa milango na madirisha, utengenezaji wa madhabahu, upakaji wa rangi nk
Dada Lulu Mengelea akiwa na mheshimiwa naibu waziti wa katiba na sheria Angela Kairuki.Kulia kwa naibu waziri ni bwana Matemba.Nyuma ni katibu mkuu wa usharika wa Mwenge mzee Kombe
Washarika mbalimbali wakifuatilia ibada hiyo
Baadhi ya washarika wakiwa kwenye ibada hiyo
Kwaya mbalimbali zilihudumu kwenye ibada hiyo.Juu ni kwaya ya Winners ya Ubungo ikiimba kwenye harambee hiyo
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi wakijadili jambo nje ya kanisa.Kutoka kushoto ni dada Lulu Mengele Maro, bwana Maro na bwana Silaa
Kwaya ya Umoja ya Usharika wa Mwenge ikihudumu kwenye ibada hiyo.Kwaya hiyo inaongozwa na mwalimu Kayese
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya harambee.Kutoka kulia ni mzee Lema, Mzee Uronu, bwana Kileo na mdau ambaye jina halikupatikana
wa Dayosisi akiwepo mkuu wa kanisa Dr Malasusa.Hakika ilikua ni ibada ya aina yake
Pia ilikuwepo kwaya ya wainjilisti na parish workers.Pichani ni parish worker wa Usharika wa Mwenge parish worker Suzan Mwimbe akiongoza kwaya hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee mzee Davis Chonjo akihojiwa na waandishi wa habari wa Itv na Redio One
Pia ilikuwepo kwaya ya wazee wa kanisa ambao nao walitia fora kwa uimbaji wao
Bwana Matemba (ambae pia alikua Mc wa harambee hiyo) akiongoza kwaya ya wazee wa kanisa
Wageni mbalimbali wakitambulishwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge (hayupo pichani)
Mheshimiwa naibu waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki katikati akiwa kwenye ibada hiyo.Kushoto kwake ni bwana Matemba ambaye pia alikua Mc wa harambee hiyo ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya Winners ya Magomeni.
Kutoka kushoto mkuu wa jimbo la Kaskazini mchungaji Muro, msaidizi wa askofu mchungaji Fupe na mkuu wa kanisa Dr Alex Malasusa
Wachungaji mbalimbali wakifanya utambulisho kwenye ibada hiyo
Naibu waziri wa Katiba na Sheria mheshimiwa Angela Kairuki akiongea kwenye ibada ya harambee hiyo.Naibu waziri alisisitiza viongozi wa dini kuhubiri na kuombea amanai katika nchi ya Tanzania ili nchi yetu iendelee kuwa kisiwa cha amani
Vitu mbalimbali vilinadiwa kwenye harambee iyo ikiwemo pikipiki ambayo ilinunuliwa na Rachel Machunde kwa shilingi milioni tatu..Pichani mkuu wa kanisa akimpongeza dada Rachel Machunde kwa kumtolea Mungu sadaka hiyo
Ilikuwepo pia sofa seti (traditional sofa set) ambayo ilinunuliwa bwana Wiliam Ngowi kwa shilingi milioni tatu na laki mbili.Pichani bwana Ngowi akiwana mke wake wakijaribu kukaa kwenye sofa hizo za kitamaduni
Nibu waziri naye alipata nafasi ya kununua saa ya ukutani
Ndugu Kichila (mdau) naye alipata nafasi ya kununua mojawapo ya vitu vilivyoletwa kwenye harambee siku hiyo
Ndugu Assey naye akinunua mojawapo ya vitu vilivyoletwa kwenye harambee hiyo.Pembeni ni mtoto wake bwana Assey
Washarika na wageni mbalimbali wakinunua vitu mbalimbali
Dada Lulu Mengele naye akinunua baadhi ya vitu kwenye harambee hiyo
Kwaya ya Winnera ya Ubungo wakiimba kwenye harambee hiyo
Wazee wa kanisa wakiongoza waumini kutoka kwenye ibada hiyo ya harambee.Kutoka kushoto mzee mama Ngole, mzee mama Chacha na nyuma ni mzee Swai
Wachungaji wakitoka kwenye ibada hiyo
Picha ya pamoja na mkuu wa kanisa
No comments: