Latest News


More

Jinsi ya kuwalinda Watoto Wako Wasinaswe na Mtego wa Kununua Vitu Kupita Kiasi

Posted by : Unknown on : Friday, August 30, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :

Walinde Watoto Wako Wasinaswe na Mtego wa Kununua Vitu Kupita Kiasi
Matangazo ya kibiashara huwalenga hasa watoto, na kwa sababu nzuri. Vijana leo wananunua vitu vingi kuliko wakati mwingine wowote. Nchini Marekani, vijana hutumia mabilioni ya dola kila mwaka kununua vitu.

Hata hivyo, mtafiti Juliet Schor anasema kwamba ni rahisi zaidi kwa watoto ambao hununua vitu kupita kiasi kupatwa na mshuko wa moyo na wasiwasi na wana uhusiano mbaya na wazazi wao. Unaweza kuwalindaje watoto wako? Fikiria njia ambazo wazazi fulani wametumia ili kuwalinda watoto wao.

WAELIMISHE: “Huwezi kuwalinda watoto wasiathiriwe na matangazo ya kibiashara kwa sababu yako kila mahali. Kwa hiyo sisi huwaambia binti zetu kwamba mashirika yanayotumiwa kutangaza bidhaa yana lengo fulani na makampuni yaliyowaajiri yanataka kupata pesa. Hayajali masilahi yao.”—James na Jessica.

USILEGEZE MSIMAMO: “Watoto humshinikiza mzazi awanunulie kitu fulani, nao hawaachi hadi awanunulie. Lakini usikubali kushindwa. Mwishowe watajifunza kwamba si lazima wapate kila kitu wanachotaka. Tulipokuwa tukimlea binti yetu, tulizungumza pamoja tukiwa wazazi kuhusu kuwa na usawaziko na mipaka ambayo tungemwekea.”—Scott na Kelli.

PUNGUZA MUDA WA KUTAZAMA MATANGAZO YA KIBIASHARA: “Familia yetu hutumia wakati mchache sana kutazama televisheni. Si kawaida yetu kutazama televisheni. Badala ya kutazama televisheni sisi hutumia wakati huo kufanya mambo mengine. Sisi hupika na kula pamoja, na wavulana wetu hupenda sana kusoma.”—
John na Jenniffer.

No comments:

Leave a Reply