Papa Francis
Kiongozi wa kanisa la Katoliki duniani, Papa Francis
na Mfalme Abdullah wa Jordan wameafikiana wakati wa mkutano
waouliofanyika katika makao makuu ya Papa ya The Vatican kuwa mazungumzo
baina ya raia wenyewe wa Syria kwa usaidizi wa jamii ya kimataifa ndio
suluhu pekee ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Mfalme Abulla alisafiri kutoka Oman hadi Italy kukutana na Papa mpya.
Mfalme Abdulla aliambatana na mkewe Malkia Rania ambapo walikaa kwa mkutano wa fagha na Papa Fransis kwa muda wa dakika 20.
Jordan inakabiliwa na wimbi kubwa la wakimbizi wanaokimbia mzozo wa vita nchini Syria.
Taarifa iliyotolewa na Vatican baada ya ziara hiyo, haikutaja lolote kuhusu mzozo wa kimataifa ulioibuka kuhusu matumizi ya silaha za kemikali.
Taarifa hiyo ilisema kwamba Papa Francis na Mfalme Abdulla wamekubaliana kuwa njia pekee ya kutanzua mzozo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria ni kufanyika mazungumzo ya amani baina ya pande hasimu nchini humo kwa usimamizi wa jamii ya kimataifa.
Utawala wa Vatican umebainisha wazi kuwa inapinga mpango wa Marekani wa kuuadhibu utawala wa rais Bashar al Assad kwa kufanya mashambulio ya kijeshi.
No comments: