Usharika wa Sinza wa kanisa la K.K.K.T umefanya ibada ya uzinduzi wa kanisa lao jumapili hii.Ibada hiyo iliyoongozwa na mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) ASKOFU Dr.Alex Malasusa .Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nje na ndani ya nchi akiwepo askofu mkuu wa kanisa la Kilutheri la Bavaria Ujerumani askofu Heinrich Bedford Strohm.Pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa Dayosisi akiwepo msaidizi wa askofu mchungaji Fupe, wakuu wa majimbo , wachungaji mbalimbali wa sharika za dayosisi, wageni waalikwa na washarika wa Usharika wa Sinza.Mchungaji wa Usharika wa Sinza ni mchungaji Abraham Mchome (pichani juu akiwa na Askofu Dr Alex Malasusa)akisaidiana na mwinjilisti Emanuel Marko Manu na parish worker Ambokile Mwakatobe
Katika ibada hiyo iliyokuwa na wanakwaya mbalimbali kama vile ;
· kwaya ya umoja ya Sinza,
· kwaya ya watoto ya Sinza,
· kwaya ya matarumbeta ya Wazo Hill,
· kwaya ya Winners ya Ubungo na
· kwaya ya Umoja ya jimbo la kaskazini
Viongozi mbalimbali wa Dayosisi ya Masharika na Pwani wakiwa na wachungaji mbalimbali wa sharika pamojaPichani kushoto mwa askofu mkuu Dr Alex Malasusa ni msaidizi wa askofu mchungaji Fupe, kulia kwa Dr Malasusa ni askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo mchungaji Elinaza Sendoro, msaidizi wa askofu mstaafu mchungaji Yohana Marko
Kwaya ya matarumbeta ya Wazo Hill wakiongoza kuingia kwenye nyumba ya ibada tayari kuanza ibada hiyo
Mkuu wa kanisa askofu Dr.Alex Malasusa akijiandaa kufungua Usharika wa Sinza
Wachungaji mbalimbali, washarika wakimsikiliza mkuu wa kanisa Dr.Malasusa wakati akiongoza liturjia ya ufunguzi wa kanisa la Usharika wa Sinza
Mkuu wa kanisa Askofu Dr Alex Malasusa akisoma neno la Mungu wakati wa ufunguzi wa Usharika wa Sinza
Washarika mbalimbali wakifuatilia ibada ya uzinduzi wa Usharika wa Sinza.Pichani mwenye miwani ni mzee Manase mwana wa Ndanshau
Askofu mkuu wa kanisa la Kilutheri Bavaria Ujerumani mchungaji Heinrich Bedford Strohm akihubiri kwenye ibada hiyo.Pembeni yake ni mkuu wa jimbo la kaskazini mchungaji Anta Muro akitafsiri mahubiri hayo
Walikuwepo wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kama raia hawa toka Ujerumani wanavyoonekana
Askofu mstaafu wa DMP askofu Elinaza Sendoro akizungumza kwenye ibada hiyo
Kwaya kuu ya Usharika wa Sinza wakiimba kwenye ibada hiyo
Kwaya ya watoto wa shule ya jumapili wakiimba kwenye ibada hiyo
No comments: