Latest News


More

WASHARIKA WA SINZA WAWAZAWADIA VIONGOZI WAO

Posted by : Unknown on : Wednesday, August 14, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
 Washarika wa Usharika wa Sinza wa K.K.K.T jumapili iliyopita waliwazawadia viongozi mbalimbali wa Usharika wao na wazee wa kanisa ambao wamewahi kuhudumu katika Usharika Huo.Viongozi hao waliozawadiwa ni ambao wamewahi kuongoza kanisa hilo tangu kuanzishwa kwake  wakati wakisali katika shule ya msingi mashujaa mkapa kuweza kununua godown ambalo lilivunjwa na kujengwa kanisa kubwa na la kisasa
Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika katika ibada ya uzinduzi wa Usharika wao huo.Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mkuu wa kanisa la K.K.K.T Dr Alex Malasusa na viongozi mbalimbali wa Dayosisi.
Pichani juu askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo Mchungaji Elinaza Sendoro akipokea zawadi kutoka kwa mkuu wa kanisa Dr Alex Malasusa.Nyuma ni mkuu wa jimbo la Kaskazini mchungaji Anta Muro



 Mzee Manase Mwana wa Ndanshau akiwa na mke wake nao walizawadiwa zawadi.Pichani juu ni mzee Manase mwana wa Ndanshau akimpa mkono mkuu wa kanisa askofu Dr.Alex Malasusa.Pembeni ni mke wake.
Chini ni mzee Manase mwana wa Ndanshau  na mke wake wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa kanisa na pembeni ni mchungaji kiongozi wa Usharika wa Sinza mchungaji Mchome
Viongozi mbalimbali walipata zawadi kama shukrwani kwa kazi nzuri ya ujenzi wa nyumba ya bwana


















No comments:

Leave a Reply