Dar, Moshi.
Baadhi ya abiria na watu waliokuwa wakitarajia kupokea miili ya ndugu zao waliofariki dunia nje ya nchi, walikwama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya ndege za kutokea Kenya kusimamisha huduma kutokana na moto uliozuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Baadhi ya abiria na watu waliokuwa wakitarajia kupokea miili ya ndugu zao waliofariki dunia nje ya nchi, walikwama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya ndege za kutokea Kenya kusimamisha huduma kutokana na moto uliozuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Uwanja huo uliopo Nairobi ambao hutumiwa na ndege
nyingi za kimataifa kuunganisha safari zake katika nchi mbalimbali,
ulisimamisha kwa dharura safari za ndege zikiwamo za Shirika la Ndege ya
Kenya (KQ) kwa siku nzima ya jana.
Taarifa zilisema ndege zote zilizokuwa zitue
uwanja wa Jomo Kenyatta kwa siku ya jana hazikuruhusiwa, na zile
zilizokuwa tayari angani zilielekezwa kutua kwenye viwanja vya ama
Mombasa, Kenya au Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) uliopo mkoani
Kilimanjaro, Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa, chanzo cha moto huo bado
hakijajulikana, ambapo taarifa zingine zilisema kuwa moto huo ulianza
kuwaka saa 11 alfajiri na kusababisha usumbufu kwa abiria na wale
waliokuwa na shughuli zao kwenye uwanja huo.
Hata hivyo, vikosi vya Zimamoto na Uokoaji
vilifanikiwa kuuzima. Ilielezwa kuwa moto huo ulianzia katika chumba cha
Idara ya Uhamiaji kinachotumiwa na wasafiri wanaowasili.
Tukio hilo limemfanya Rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta kufika uwanjani hapo kujionea hali ilivyo akiwa ameambatana na
Waziri wa Mambo ya Ndani, Joseph Ole Lenku na Waziri wa Usafirishaji na
Miundombinu, Michael Kamau.
Kutokana na kufungwa kwa uwanja huo, marubani
wamekuwa wakielekezwa kutumia viwanja vingine, ukiwamo Mombasa, Eldoret
na Dar es Salaam (JNIA) na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe,
Uganda.
Uwanja wa JNIA
Mmoja wa abiria, Ahmad Abdul aliyekuwa anafuatilia
mwili wa jamaa yao aliyefariki dunia nchini India, alisema mwili huo
ulikuwa uwasili saa tatu asubuhi kwa Ndege ya KQ, lakini tangu muda huo
hadi mchana walikuwa hawajui mwili wa jamaa yao huyo utawasili uwanjani
hapo muda gani.
“Mwanzoni tuliambiwa wametua Mombasa badala ya
Jomo Kenyatta na jamaa zetu walikuwa hawajui mipangilio ya safari
ilivyo,” alisema na kuongeza: “Baadaye tulipata taarifa ndege za KQ
zimesitishwa, ikatuchanganya zaidi,” alisema Abdul.
Watendaji wa uwanja huo hawakuweza kupatikana
kutokana na kudaiwa kuwapo kwenye vikao kwa muda mrefu, lakini hata
hivyo, Mkuu wa Huduma ya Njia za Ndege katika Kampuni ya Kuingiza na
Kupakua Mizigo Uwanjani hapo ya Swissport, Mahmood Kisukari alisema hali
ya usafiri uwanjani hapo ni shwari
No comments: