Hafla hiyo fupi ilifanyika katika maeneo ya kanisa la Usharika wa Mwenge .Pichani juu katibu mkuu wa Usharika wa Mwenge Mzee Kombe akimkaribisha askofu Dr Malasusa kukata keki hiyo
Naibu waziri wa katiba na sheria mheshimiwa Angela Kairuki akichukua chakula kwenye hafla hiyo
Wageni mbalimbali wakichukua chakula kwenye hafla hiyo
Meza ya mgeni rasmi askofu Dr Malasusa wakipata chakula cha mchana .Kushoto kwake ni amsaidizi wa askofu Mch Fupe na kulia kwake ni naibu waziri wa katiba na sheria mh.Angela Kairuki
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mch.Kaanasia Msangi akiwakaribisha wageni na kuwaeleza dhumuni la hafla hiyo
Katibu wa baraza la wazee la Usharika wa Mwenge mzee Kombe akimkaribisha mgeni rasmi kwenye hafla ya kumpongeza kuwa mwenyekiti wa CCT
Wageni mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo ambayo ilikua pia na tendo la ukataji wa keki (ndafu)
Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya kumpongeza mkuu wa kanisa la K.K.K.T askofu Dr Alex Malasusa
Askofu Dr Malasusa akikata keki hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kumpongeza
Askofu Dr Malasusa akifurahia keki hiyo baada ya kuila.Kushoto kwake ni naibu waziri Mh.Angela Kairuki, katibu wa Usharika wa Mwenge mzee Kombe na mama Palangyo ambaye naye ni mzee wa Usharika wa Mwenge
Naibu waziri mh.Angela Kairuki naye akifurahia keki hiyo
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge naye akifurahia keki hiyo.Pembeni ni mgeni rasmi askofu Malasusa akiwashukuru washarika wa Mwenge kwa kumwandalia hafla hiyo ya kumpongeza
No comments: