SHUKRANI ZETU
Ibada ya jumapili hii iliyofanyika katika usharika wa Mwenge (K.K.K.T) .Ibada hiyo iliyoongozwa na Mwinjilisti wa Usharika Mwinjilisti Mwigune na mahubiri yaliongozwa na mchungaji Mchomvu wa Kijichi akisaidiana na mchungaji mstaafu Heriel Mfinanga wa Usharika wa Kijihi
Neno la Waraka lilisomwa na Mzee wa Kanisa mzee T.kichila
Matangazo yalisomwa na mzee Uronu
Neno la waraka: Luka 2:22-24
Neno Kuu 2Korintho 8:1-5
Akihubiri katika ibada hiyo mchungaji Mchomvu (pichani juu) alisema shukrwani ni tendo linalofanyika baada ya mtu au watu kufanyiwa jambo zuri au lililomrithisha
Mtume Paulo anatoa ushuhuda kwa kanisa la Makedonia abao walipatwa na majanga ya ukweli lakini pamoja na yote bado waliendelea kumshukuru Mungu bila kuchoka
Hivyo hata sasa sisi tunapaswa kumshukuru Mungu wakati wowote bila kujali tunapatwa na mambo mazuri au la, alihubiri mchungaji Mchomvu
Mahubiri hayo yalifanyika katika ibada ya kwanza katika Usharika wa K.K.K.T Usharika wa Mwenge
Kwaya mbalimbali zilihudumu kwenye ibada hiyo ikiwepo kwaya ya Uinjilisti , kwaya ya Vijana na kwaya ya watoto wa Mungu kutoka Usharika wa Hananasif, Kinondoni.Pichani juu kwaya ya Uinjilisti ikiimba
No comments: