Jumapili hii ilifanyika ibada nzuri katika Usharika wa K.K.K.T – Mwenge
Katika ibada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji wa Usharika huo Mchungaji Kaanasia Msangi na mahubiri yaliongozwa na Mwinjilisti wa kujitegemea Ernest Munis (pichani juu).
Ndugu Munis ni msharika wa Magomeni na kiongozi wa Fellowship wa Usharika wa Magomeni na pia ni kiongozi wa Fellowship wa jimbo la Kaskazini
Neno kuu lilitoka Mathayo: 12: 1 – 8
Neno la Waraka: Yakobo: 2:8-13
Akihubiri katika ibada hiyo Mwinjilisti Munis alisema Ukristo sio kifungo/utumwa Fulani, bali ni uhuru ndani ya Kristo
Huru maana yake ni kutokua mtumwa wa kitu au kifungo chochote
Kuzaliwa kwa Yesu; kufa kwake na hata kufufuka kwake kulikua ni kumfanya Mristo aweze kuwa huru.Huru katika biashara;kilimo;alie mfanyakazi awe huru;taifa liwe huru; huru katika kila kitu alisema bwana Munis
Mungu hatamani mkristo awe mtumwa wa jambo lolote lile,na hili Mungu alilianza kwenye taifa la Israel kwa kuwatoa katika Utumwa wa Misri
Uhuru wa Yesu unafungua ndoa zilizofungwa, magonjwa yaliyoko ndani yako n.k
Mungu anawatazama Wakristo katika viwango vya tofauti kabisa na walivyo waxhawi au wanga
Mungu mar azote anatuwazia mambo yaliyo mema tu wakati wowote
Mathayo 12:1-8
MAMBO YANAYOWEZA KUMFUNGA MKRISTO;
1.Mashamba /Mazingira
2.Maombi – omba kwa bidii na ukiomba utapewa
3.Imani
Tukiweza kujinasua katika maeneo hayo tutatembea tukiwa huru na hakuna kuwa tena kwenye mateo au kifungo chochote alimalizia mahubiri yake bwana Munis
Waumini wakiimba kwa hisia nyimbo za kusifu na kuabudu kwenye ibada hiyo ya jumapili
Waumini mbalimbali pichani juu na chini wakiabudu kwenye ibada hiyo ya jumapili
Picha juu na chini ni waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti wakihudumu kwenye ibada hiyo ya jumapili katika Usharika wa Mwenge
Ibada hizo zilifanyika mbili, moja ilianza saa moja kamili na ya pili ilianza saa nne kamili asubuhi
No comments: