Latest News


More

SIMBA AMUUA MFANYAKAZI HUKO ETHIOPIA

Posted by : Unknown on : Tuesday, September 24, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
Simba amuua mfanyakazi Ethiopia
Mfanyakazi mmoja wa hifadhi ya wanyama amefariki baada ya kushambuliwa na Simba katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, baada ya kusahau kufunga lango la chumba cha mnyama huyo.

Simba huyo anayeitwa Kenenisa, ambalo ni jina la mwanariadha mashuhuri Kenenisa Bekele, alimuuma Abera Silsay, 51, shingoni, wakuu wa hifadhi hiyo wanasema.

Shambulio hilo linasemekana kudumu kati ya dakika 15-20

Hifadhi hiyo ilifunguliwa mwaka wa 1948 kuwalinda Simba waliokuwa wamefugwa na kiongozi wa zamani wa Ethiopia, Haile Selassie.

Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza akiwa mjini Addis, anasema alipozuru hifadhi hiyo saa kadhaa baada ya tukio hilo la Jumatatu asubuhi, kiatu cha mwanaume huyo aliyeuwawa kilikuwa bado kwenye sakafu, kando ya Simba huyo mwenye umri wa miaka saba.

Hifadhi hiyo ilifungwa siku nzima kwa umma. Maafisa wanasema takriban watu 2000 hutembea hapo kila siku.

Walinzi walijaribu kumshutua Simba huyo kwa kufyatua risasi hewani lakini juhudi zao ziliambulia patupu, mwandishi wetu anasema.

Bwana Abera alishambuliwa alipokuwa akisafisha chumba cha simba huyo

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Dkt Musie Kiflom anasema mfanyikazi huyo alikuwa amedumu kwa mwaka mmoja tuu katika kazi hiyo na hakuwa na uzoefu mkubwa ikilinganishwa na wafanyakazi wenzake.

"Aliingia chumba nambari 10 ambapo Kenenisa hulala na alisahau kufunga lango la chumba anakolala simba huyo” Musie Kiflom aliliambia shirika la habari la AFP.

"hatimaye, simba huyo alikuja na kumvamia," alisema.

Bwana Musie aliwaambia wanahabari kuwa polisi waliitwa kujaribu kusaidia, lakini ilikuwa “ vigumu sana kumsaidia mwenzetu”.

Bwana Abera alifariki papo hapo, aliongezea.

Hifadhi hiyo ni makao ya simba 15 wa Uhabeshi, ambao wamo hatarini

Simba hao huwekwa katika nyumba zilizofungwa lakini wakuu wanasema mipango inaendelea kuwahamisha hadi nyingine ambayo ni kubwa zaidi katika miezi 13 ijayo.

Hii ni mara ya pili kwa mfanyakazi wa kutunza simba katika kituo hicho katika kipindi cha miaka 17, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Hifadhi hiyo sasa itaimarisha mafunzo kwa wafanyikazi wote baada ya tukio hilo.

No comments:

Leave a Reply