Latest News


More

WAALIMU WAWILI NDUGU WAFANYA VIZURI MASHINDANO YA UIMBAJI K.K.K.T JIMBO LA KASKAZINI

Posted by : Unknown on : Wednesday, October 23, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
 Waalimu wawili ndugu, Erick Lwiza na Kennedy Lwiza wamefanya vizuri katika mashindano ya uimbaji yaliyofanyika jumamosi iliyopita katika Usharika wa Mbezi Beach Jimbo la Kaskazini
Ndugu hao ambao wanafundisha kwaya za Usharika wa Kinondoni (mwalimu Kennedy Lwiza) na kwaya kuu ya Usharika wa Ubungo (mwalimu Erick Lwiza)

 Wakizungumza na mtandao huu wa tumainiletu jumamosi iliyopita kanisani hapo walisema wao ni ndugu na Kennedy (pichani juu kushoto aliyevaa kaunda suti) ndie mkubwa na Erick (kulia mwenye tai )ni mdogo
 Katika mashindano hayo Mdogo mtu Erick ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kwaya yake ya Usharika wa Magomeni kuibuka kidedea kwa kuchukua nafasi ya kwanza, huku kaka yake Kennedy aliongoza kwaya yake ya Usharika wa Kinondoni kuchukua ushindi wa pili.Mshindi wa tatu alikua kwaya kuu ya Usharika wa Mbezi Beach
 Pichani juu mwalimu Kennedy wa Usharika wa Kinondoni akimpa mmoja wapo wa majaji wa shindano hilo mkono wakati wa kupokea zawadi jumamosi iliyopita.Nyuma yake ni kiongozi wa kwaya kuu ya Usharika wa Kinondoni
Pichani juu mwalimu Erick wa kwaya ya Usharika wa Magomeni akimpa mkono mmojawapo wa majaji wakati wa kupokea zawadi.Nyuma yake ni kiongozi wa kwaya kuu ya Usharika wa Magomeni
Saved under :

No comments:

Leave a Reply