Swali: "Ni kwa nini Mungu aliichagua Israeli kuwa watu lake wateule?"
Jibu: Kuzungumzia taifa la Isreali, Kumbumbuku La Torati 7:7-9 yatuambia, “BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sabau mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawaatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kusika amri zake, hata vizazi elfu.”
Mungu alilichagua taifa la Israeli kuwa watu ambao kupitia kwao Yesu Kristo atazaliwa- mwokozi kutoka kwa dhambi na kifo (Yohana 3:16). Mungu kwanza aliahidi Masia baada ya Adamu na Hawa kuanguka katika dhambi ( Mwanzo mlango wa 3). Mungu baadaye alithibitisha kuwa Masia atakuja kutoka kwa uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo (Mwanzo 12:1-3). Yesu Kristo ndiye sababu kuu ya Mungu kuichagua Israeli kuwa watu wake malaamu. Mungu hakustahili kuwa na watu wateulie, lakini aliamua kufanya namna hiyo. Yesu alistahili kukuja kutoka kwa taifa la watu fulani na Mungu akachagua Israeli
Ingawa, sababu ya Mungu kuichagua taifa la Israeli halikuwa peke lengo la kumtoa Masia. Nia ya Mungu kwa Israeli ilikuwa kwamba wataenda na kuwafunza wengine kumhusu. Israeli ilikuwa iwe taifa la makuahani, manabii na wamisionari kwa ulimwengu. Nia ya Mungu ilikuwa, Israeli iwe watu wa kipekee, taifa ambalo lingeelekeza wengine kwa Mungu na ahadi zake, kutolewa kwa mkombozi, Masia na mwokozi. Kwa sehemu nyingi Israeli ilikosea katika jukumu hili. Hata hivyo lengo lake kabisa kwa Israeli- lile la kuleta Masia katika ulimwengu- lilitimizwa kikamilifu katika Kristo Yesu.
No comments: