Wengi hawazingatii utunzaji wa kifaa hiki muhimu katika usafi wetu wa kila siku.
Mswaki wako umejaa vijidudu visivyoonekana kwa macho (bakteria) hiyo ni kwa mujibu wa watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Manchester Uingereza.
Wamegundua kuwa mswaki mmoja usiofunikwa una uwezo wa kubeba bakteria zaidi ya milioni 100 wakiwamo E. coli wanaoweza kusababisha magonjwa ya kuhara na staphylococci wanaosababisha maambukizi katika ngozi.
“Kimsingi kuna mamia ya bakteria kwenye midomo yetu ambao huzaliana kila siku,” anasema Gayle McCombs, kutoka kwenye kituo cha utafiti cha afya ya meno cha kilichopo kwenye Chuo Kikuu cha Old Dominion.
“Hilo halina shida. Tatizo hutokea pale idadi kubwa ya bakteria wasio salama kiafya watakapoingia mdomoni” anasema McCombs.
Anasema ule utando unautoka kwenye meno wakati wa kupiga mswaki ni bakteria.
“Kwa kadri unavyopiga mswaki unakuwa katika nafasi ya kujaza mamia ya bakteria kwenye mswaki wako, ” anasema Dk Harms.
Unaweza kukusababishia maradhi
Wakati mwingine kulingana na kiwango cha bakteria waliopo kinywani mwako au wale walioingia kupitia mswaki wako, kinga yako ya mwili ya asili huwa imejiweka tayari kupambana na maradhi yoyote yatakayosababishwa na bakteria.
“Kwa bahati nzuri mwili wa mwanadamu wenyewe una uwezo mkubwa wa kupambana na bakteria anasema Kimberly Harms.
Anasema, “Hata hivyo hatuna uhakika ikiwa kwa kuuweka mswaki wako bafuni kwenye kasha la miswaki, kunaweza kusababisha matatizo yanayoweza kudhuru afya yako.”
Lakini bado unahitaji kutumia akili yako hasa pale unapohifadhi mswaki wako. Jaribu kuweka sehemu safi na salama. Epuka kuweka mswaki wako chooni.Hata kama unaweka mswaki wako bafuni, kumbuka kuwa vyumba vingi vya mabafu huwa ni vidogo. Tena viko karibu kabisa na vyoo.
No comments: