NDOA ZA PAMOJA KUFUNGWA KESHO KANISA LA K.K.K.T USHARIKA WA MWENGE
Posted by :
Unknown
on :
Saturday, November 23, 2013
0 comments
Kesho katika kanisa la Kiinjili la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Mwenge kutafungwa ndoa za pamoja zipatazo tisa
Akizungumza wakati wa mazoezi na maharusi yakiwa ni maandalizi ya ndoa hizo Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi amesema ndoa hizo zitafungwa katika ibada ya pili itakayoanza saa nne kamili asubuhi
Baada ya ibada kutakua na sherehe ya kuwapongeza maharusi katika viwanja vya kanisa ambapo washarika pamoja na ndugu na jamaa wa maharusi watajumuika pamoja kula na kunywa
Pichani juu na chini mchungaji Kaanasia Msangi akitoa mafundisho ya mwisho wakati wa mazoezi hayo
Maandalizi ya kupanga sehemu ya kufanyii sherehe hiyo yakiendelea kwa kupamba
Maharusi watarajiwa wakiwa ibadani wakiendelea na mazoezi
Mchungaji kiongozi akiendelea na mazoezi kanisani
Maharusi wakifanya mazoezi ya kuvishana pete
Sherehe hiyo ambayo imeandaliwa na washarika wa Mwenge itafanyika kuanzia saa saba mchana mara baada ya ibada ya ndoa
Akizungumza na mtandao huu mchungaji wa Usharika huop alisema ni mara ya kwanza kwa Usharika kuandaa ndoa za pamoja na kufanya sehrehe moja kwa wanandoa
Hii ni historia kwa Usharika wetu wa Mwenge na nawakaribisha wakristo wote kuhudhuria na kujumuika pamoja na wanadoa wetu, alisema mchungaji Kaanasia Msangi
No comments: