Latest News


More

NDOA ZA PAMOJA ZAFUNGWA LEO KATIKA KANISA LA K.K.K.T - USHARIKA WA MWENGE

Posted by : Unknown on : Sunday, November 24, 2013 0 comments
Unknown

NDOA ZA PAMOJA ZAFUNGWA LEO KANISA KA K.K.K.T – USHARIKA WA MWENGE


Leo jumapili katika Usharika wa kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge zimefungwa ndoa nane kwa pamoja
Katika ibada hiyo ndoa zilizofungwa ni ndoa kati ya
1.Bwana Paulo Muhamed Myenga na Bi Linnah Raphael Mkemangwa
2.Bwana Hans Elias Mgalike na Bi Lilian Selestine Kafrika
3.Bwana Florence Philemon Assey na Bi Matilda August Kessy
4.Bwana Alex Marubiri Kong'a na Bi Theresia James Paulo
5.Bwana AngeloElia Mwakambinda na Bi Lenzia Godfrey
6.Bwana Goodluck Ezekiel Mmary na Bi Neema Emilian Massawe
7. Bwana Albert Ernest Moshi na Bi Davita Ringia Swai na
8.Bwana Allen Ally Juma Makatta na Bi Beatrice Simon Mwamakubi

Pichani juu na chini maharusi wakiingia ibadani tayari kuanza ibada hiyo ya ndoa
 Maharusi wakiingia ibadani huku wakiongozwa na kikundi cha matarumbeta kinachoongozwa na mwalimu
Kayese
Kila ndoa waliingia na wadhamini wao




 Bwana Angelo Elia Mwakambinda na bi Lenzia Godfrey wakiingia ibadani na wapambe wao
 Bwana Allen Allly Juma Makatta na Bi Beatrice  Simon Mwamakubi wakiingia ibadani
 Bwana Florence Philemon Assey na bi Matilda August Kessy wakiingia ibadani na wapambe wao
 Bwana Goodluck Ezekiel Mmary na Bi Neema Emilian Massawe wakiwa na wasimamizi wao wakiingia ibadani
Wazee wa kanisa wakiongoza msafara kuingia ibadadi.Wazee waliohudumu katika ibada hiyo ni mzee Kihunrwa, Mzee mama Ndossi, Mzee mama Chonjo na mzee Lema
Awali kabla ya kuingia ibadani maharusi walipata wasaa  wa kupewa machache na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge jinsi ibada itakavyokua
Pichani chini mchungaji Kaanasia akizungumza na maharusi hao

Maharusi pichani chini wakimsikiliza mchungaji Kaanasia (hayupo pichani)
Pichani juu ni wanandoa hao wakiwa kwenye maandalizi ya kuingia ibadani.
Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akisaidiwa na mchungaji Fue wa Same

Katika Ibada hiyo iliyokuwa na waumini wengi na ndugu na jamaa wa marafiki ilikua pia na ushiriki wa chakula cha bwana

Baada ya kufunga ndoa maharui hao waliandaliwa sherehe ya aina yake katika viwanja vya kanisa na kuhudhuriwa na waumini wa Usharika huo pamoja na ndugu na jamaa wa maharusi

Hakika lilikua ni tukio la kipekee katika Usharika huo wa Mwenge
Picha zaidi kufuata..................................

No comments:

Leave a Reply