Johannesburg, Afrika Kusini.Rafiki wa karibu wa familia ya Nelson Mandela, Bantu Holomisa amesema madaktari walikata tamaa kiongozi huyo na kumwondolea mashine ya kupumulia na kufariki dunia baada ya saa mbili.
“Alionekana ametulia kana kwamba amelala na hiyo ilionyesha kuwa madaktari walikuwa wameshakata tamaa na wamefikia mwisho wa kupigania maisha yake,” alisema Holomisa na kukaririwa na Shirika la Habari la AP.
Rafiki huyo wa Mandela ambaye alikuwa na familia hiyo kabla na baada ya Mandela kutoka gerezani mwaka 1990, aliiambia AP kwamba aliitwa na wanafamilia hasa baada ya hali ya Mandela kubadilika na kuwa mbaya zaidi.
Holomisa alisema alipofika nyumbani, alikuta wanandugu 20 wamekusanyika wakiwa wamemzunguka. “Niliona watu wakiwa wanahangaika naye na nilijua tu kuwa sasa imefikia hatua ya mwisho... baada ya saa mbili, Mandela alifariki dunia.”
No comments: