KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA YAZINDUA LOGO YAO LEO
Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama maarufu kama Kijito leo imezindua logo yao ambayo itatumika katika kila bidhaa ambayo watakuwa wanaiuza.Logo hiyo kama inavyoonekana hapo juu imezinduliwa leo katika ibada iliyofanyika usharikani hapo
Akizungumza katika uzinduzi wa logo hiyo mwenyekiti wa kwaya hiyo (pichani juu) amesema wamekua wakiuza bidhaa mbalimbali ambazo hazina nembo maaluma lakini kuanzia sasa kila bidhaa watakayoiuza itakua na nembo yao hiyo
Baadhi ya bidhaa ambazo wameanza kuziuza kwenye ibada hiyo ni pamoja na Mug ya kunywea chai ambayo imewekwa logo yao hiyo mpya
Katika uzinduzi huo waliuza Mug hizo takriban 30 ambazo zilipatikana pesa taslimu na ahadi zaidi ya shilingi milioni moja
Katika uzinduzi huo kwaya ya Tumaini ya Arusha pia ilihudhuria kama kwaya rasmi alikwa
Wanakwaya ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakishikilia vikombe ambavyo vina logo yao mpya
Wanakwaya ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakiimba wimbo maalum wenye maana ya logo yao Kijito
Mchungaji wa Usharika wa Kijitonyama mchungaji Kadiva akiweka wakfu logo ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama akiwapa mkono washarika waliokuwa wa kwanza kununua vikombe vyenye nembo ya Kijito.Vikombe hivi viliuzwa kuanzia shilingi 10,000 mpaka shilingi 200,000

No comments: