Latest News


More

KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA KUFANYA TAMASHA KUBWA LEO LA JUBILEE YA MIAKA 25

Posted by : Unknown on : Sunday, December 8, 2013 0 comments
Unknown
Kwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama maarufu kama Kijito leo jumapili watafanya tamasha lao la kumbukumbu ya miaka 25

Tamasha hilo lotafanyika kanisani hapo katika Usharika wa Kijitonyama.Tamasha hilo litaanza saa nane mchana na kuendelea ambapo kwaya mbalimbali za usharika huo zitashiriki ikiwepo kwaya ya Uamsho , kwaya ya Vijana , Kwaya rasmi ya Tumaini toka Arusha na kwaya nyingine mbalimbali.


 Pichani juu na chini wanakwaya ya kwaya ya Tumaini toka Arusha wakiimba kwenye ibada hiyo maalum ya miaka 25 ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama


 Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo
 Waimbaji wa matarumbeta wakiimba wakati wa kuanza ibada hiyo ya jumapili
 Juu na chini wanakwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama wakiimba kwenye ibada hiyo
Akiwakaribisha wakristo kushiriki tamasha hilo mchungaji kiongozi mchungaji Kadiva alisema ni jambo la
kuwapongeza kwaya hiyo kwa kuweza kumwimbia bwana kwa kipindi chote hicho bila kukata tama

Nawaombeni washarika wa Mwenge na marafiki zenu mje kwenye tamasha hili leo mchana kwani ndio njia pekee ya kumrudishia mungu utukufu kwa kazi njema wanayofanya kwaya hii ya Kijitonyama alisema mchungaji Kdiova

No comments:

Leave a Reply