MAHAFALI ST.DON BOSCO YAFANA DAR ES SALAAM
Mahafali ya 18 ya shule ya awali ya ST.Don Bosco yamefanyika
jana jumamosi na kufana sana.Mahafali hayo yalifanyika katika viwanja vya shule
hiyo maeneo ya Sinza karibu na kanisa la Full Gospel Bible Fellowship
Katika mahafali hayo takriban watoto 36 walihitimu ambao
mwakani wataingia shule ya msingi
Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikua Bwana Arnold ambaye
ni mwenyekiti wa kanisa la Roman Catholic parokia ya Sinza
Akimkaribisha mgeni rasmi, mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo
bwana David Mfanga alisema shule hiyo inapata mafanikio kila mwaka kwani
wanafunzi wanaongezeka kila mwaka ambapo
kwa sasa hivi shule ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 kwa wakati mmoja
Awali mwaliku mkuu wa shule hiyo alisema shule hii ilianza
rasmi mwaka 1995 Januari ikiwa na wanafunzi 40 tu .Hivi sasa shule ina uwezo wa
kuchukua wanazunzi 120 kwa wakati mmoja alisema mwalimu huyo.Mikakaiti iliyopo
sasa ni kujenga shule ya msingi ambapo kiwanja kimepatikana maeneo ya Mvuti na
tayari mchoro wa ramani ya shule hiyo
uko tayari
Shule ya Don Bosco inafundisha masomo yafuatayo;
English, Hesabu, Kiswahili, Sanaa, Afya, Dini na
Maadili.Masomo yote yanafundishwa kwa kiingereza isipokuwa Dini na Kiswahili
Shule hii inapokea wanafunzi wa umri wa miaka 2 na nusu
mpaka miaka 5 alisema mkuu huyo wa shule.
Changamoto walizo nazo kwa sasa hivi ni kupata fedha za
kuchimba kisima cha maji shuleni hapo
Katika mchango wa papo kwa papo uliochangwa ukiongozwa na
mgeni rasmi aliyetoa ahadi ya shilingi 500,000 wazazi na walezi walichangia na
kupata zaidi ya shilingi milioni moja na laki tatu ambazo ni taslimu na ahadi
No comments: