Leo ni sikukuu ambayo dunia nzimainaadhimisha kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristo
Kuzaliwa kwake kulikua tofauti sana na kuzaliwa kwa watu wengine na watu wengi walifurahi kuzaliwa kwake.Akihubiri katika ibada ya Kristmas jumatano hii katika kanisa la K.K.K.T - Usharika wa Mwenge mchungaji Juliana wa Dayosisi ya Konde alisema Kristmas ni siku muhimu sana kwa Wakristo kwani ni siku tunapokumbuka kupata ukombozi wa Mkristo
Lakini pia wako waliochukia/kukasirishwa na kuzaliwa kwa Yesu Kristo wakiwepo Wayahudi kama mfalme Herode, akijua Yesu Kristo atakuja kuchukua ufalme wake.Kumbe Ufalme wa Yesu haukuwa wa dunia hii, alisisitiza mchungaji Juliana
Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akisaidiana na mwinjilisti wa Usharika mwinjilisti Mwigune
No comments: