Latest News


More

Neslon Mandela: Atakumbukwa vipi? Angalia picha mbalimbali na wasifu wa Mzee Mandela

Posted by : Unknown on : Tuesday, December 10, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :

Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mwafrika mweusi wa Afrika Kusini,baada ya vita vya muda mrefu dhidi ya utawala wa kizungu.



Alizaliwa mkoani Eastern Cape, lakini baadaye akatorokea mjini Johannesburg ambako alifanikiwa kuwa mwakili na kujiunga na haratakati za chama cha ANC dhidi ya utawala wa kizungu.


Kama kijana, Mandela alipenda masumbwi. ''Masumbwi ni bure, Ukiwa ulingoni , umri na hadhi yako pamoja na mali yako sio muhumu,'' aliandika katika kitabu chake kuhusu maisha yake

Mwaka 1956, alituhumiwa kwa kosa la uhaini kwa sababu ya kazi yake na ANC. Wakati wa kesi yake, alikutana na mfanyakazi wa kijamii aliyeitwa, Winnie Mandela. Ndao yake kwa Evelyn Mase iliisha baada ya wawili hao kutalakiana.

Nelson na Winnie walioana mwaka 1958 lakini hawakufurahia maisha yao ya ndoa kwani wote walikuwa wakikamatwa mara kwa mara.

Nelson na Winnie walioana mwaka 1958 lakini hawakufurahia maisha yao ya ndoa kwani wote walikuwa wakikamatwa mara kwa mara.

Sura ya Mandela ikawa sasa iishara ya kampeini hiyo kote duniani


Hatimaye zaidi ya miaka ishirini baada ya kufungwa jela, Mandela aliachiliwa mwaka 1990.


Kufuatia kuachiliwa kwake, Mandela lizuru nchi nyingi na kukutana na viongozi wa dunia alipokuwa anjiandaa kuwania urais. Anaonekana hapa katika ubalozi wa Afrika Kusini mjini London ambako maandamano ya kupinga utawala wa kizungu daima yalikuwa yakifanyika.

Uchaguzi wa kwanaza wa kidemokrasia ulifanyika tarehe 27 mwezi Aprili m,waka 1994. Waafrika weusi walipanga foleni kupiga kura kwa mara ya kwanza. Chama cha ANC kilishinda uchaguzi huo kwa wingi wa kura na hivyo Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi kuongoza Afrika Kusini

Mandela alitawala nchi hiyo kwa muhula mmoja pekee na mnamo mwaka 1999 akawa mmoja wa viongiozi wachache wa Afrika kuachia ngazi kwa hiari. Thabo Mbeki, alipewa jukumu la kumrithi Mandela kama rais na kiongozi wa ANC

Baada ya kutalakiana na mkewe Winnie , Mandela alimuoa Graca Machel, alipokuwa anasherehekea miaka 100m mwaka 1998. Bi Machel ni mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji Samora Machel. Bi Graca na Mandela walianzisha hazina ya kuwasaidia watoto wasio na uwezo mkubwa maishani
 
Pia ana mambo mawili ambayo sio kawaida kwa viongozi wa dunia kuwa nayo....mpole na mwenye kuweza hata kujicheka , hapa anakutana na mwanamfalme Prince Charles na wanamuziki wa iliyokuwa bendi ya Spice Girls
Bwana Mandela, aliweza kujitokeza wakati wa sherehe ya kufunga michuano ya kombe la dunia mwaka huo. Hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya na alikuwa anaomboleza kifo cha kitukuu wake aliyeuawa huku michuano hiyo ikianza.

(Picha na habari kwa hisani ya BBC Swahili)

No comments:

Leave a Reply