Usalama wa milele wa Mkristo ni pale ambapo anakua katika kumtii na kumtumikia Mungu katika maisha yake yote.
Akihubiri katika ibada ya jumapili ya jana katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge mchungaji kiongozi wa usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi (pichani juu) amesema maandiko yanasema kwamba maisha ya mkristo ni mkristo mwenyewe anavyotaka yawe
Alisema kuna mambo matatu makuu ambayo ni;
1.Maandiko pekee yake na nguvu iliyoko katika neno la Mungu inatuokoa
2.Wokovu wa neema tunaupata kwa imani peke yake
3.Neema peke yake inaokoa
Kwa huruma za Mungu tu sisi wenyewe hatustahili ila kwa huruma yake tunaupata wokovu bure
Msamaha wa dhambi unapatikana kwa;
1.Kwa mtu akiwa na mkristo mwenzake na akakubali kuungama dhambi zake
2.Kwa mtu mwenye dhambi akiwa na kiongozi wa kiroho kama mchungaji au mwinjilisti akakubali kuungama dhambi zake
3.Kwa mtu mwenye dhambi kukiri pamoja na kiongozi wa kiroho kumtangazia msamaha
Kila mtu anamhitaji Mungu kwani wote tu wakosaji mbele za Mungu
Mungu alitoa amri kuu kumi kwa nia njema , ili ziwe mwongozo wa dira ya mwanadamu katika kuishi
Hizi ziliwekwa kwa ajili ya wanadamu wote wakati sheria za Mungu ziliwekwa na Mungu kwa ajili ya wana wa Istrael alihitimisha mchungaji Kaanasia
Pichani juu na chini waumini wakiwa kwenye ibada ya jumapili hiyo jana
Waimbaji wa kwaya ya Uinjilisti wa Usharika wa Mwenge pichani juu na chini wakihudumu kwenye ibada hiyo
Waumini waliohudhuria ibada hiyo ya jana jumapili
Waimbaji wa sifa wa Usharika wa Mwenge wakiimba kwenye ibada hiyo
Mchungaji Msangi akiimba kwenye ibada hiyo
Mchungaji Kaanasia Msangi pamoja na Mwinjilisti Mwigune wa Usharika wa Mwenge wakiimba kwa hisia kwenye ibada hiyo
Ibada hiyo pamoja na mambo mengine ilikua maalum ya kusifu na kuabudu ambapo vikundi vyote vya Usharika wa Mwenge vilishiriki
No comments: