Mhubiri aliyedaiwa kueneza itikadi kali za kiisilamu nchini
Kenya Abubakar Shariff anayejulikana kwa jina lingine kama Makaburi,
ameuawa.
Duru zinasema kuwa Makaburi aliuawa katika mtaa wa Shanzu mjini Mombasa
ambako alikuwa anaishi.
Polisi wamekuwa wakimtuhumu Makaburi kwa kueneza itikadi kali za kiisilamu
miongoni mwa vijana wa kiisilamu mjini Mombasa Pwani ya Kenya na kuchochea
vitendo vya kigaidi.
Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana kuenda kupigania kundi la
wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, madai ambayo Makaburi amekuwa
akiyakanusha.
Duru zinasema kuwa vijana wameanza kuzua vurugu katika msikiti wa Majengo,
Mombasa kufuatia taarifa za mauaji ya mhubiri huyo mwenye utata.
Taarifa za kifo cha Makaburi zilitolewa katika msikiti Musa ambao umekuwa
kitovu cha vurugu kati ya maafisa wa usalama na vijana wanaodaiwa kuhubiri na
kufuata ikitakadi kali za kiisilamu.
Haijulikani ni nani aliyemuua Makaburi
No comments: