Polisi nchini India wanasema watu kama 89 wamekufa kwenye
mkanyagano katika sherehe ya Kihindu.
Maelfu ya waumini walivuka daraja nyembamba kufikia hekalu la Madhya
Pradesh.Afisa wa eneo hilo alisema watu wengi walijeruhiwa na waokozi wanatafuta miili mtoni.
Polisi wanasema msongamano ulianza kulipozuka tetesi kwamba daraja ilikuwa inakaribia kuporomoka.
Lakini mashirika ya habari ya huko yanasema chanzo ni polisi kuanza kutumia virungu, kudhibiti umati.
Mikanyagano kama hiyo hutokea mara kwa mara nchini India katika sherehe za kidini ambazo huwa na mtafaruku
No comments: