TANGAZO USHARIKA WA MAGOMENI
Mchungaji wa Usharika wa Magomeni na Ofisi yake akishirikiana na Baraza la Wazee pamoja na Washarika wa Magomeni Mviringo wanakualika katika Ibada maalumu ya uwekaji wa jiwe la Msingi na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya linaloendelea kujengwa.Picha ya juu ni ramani ya kanisa litakavyokuwa pindi litakapomalizika
Ibada hiyo itafanyika siku ya Jumapili tarehe 12/05/2013 itaongozwa na Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili laKilutheri Tanzania na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Ibada itakuwa moja na itaanza saa mbili kamili asubuhi.
Kwaya zitakazo hudumu siku hiyo ni:
· Muungano wa Kwaya za KKKT Usharika wa Magomeni Mviringo
· Kwaya kuu KKKT Usharika wa Msasani.
· Kwaya ya Matarumbeta KKKT Usharika wa Wazo Hill.
Aidha wanafamilia wa zamani wa Usharika wa Magomeni; mliopata kuhudumu na mliopata huduma mbalimbali za Kiroho na kimwili katika madhabahu ya Magomeni mnakaribishwa sana.
Kumbuka, ni Ibada maalumu ya uwekaji wa jiwe la Msingi na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya KKKT Usharika wa Magomeni, siku ya Jumapili tarehe 12/05/2013 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.
Wanamagomeni wanasema si kwamba wamekwisha kufika ila wanakaza mwendo. Pia, unaweza kuchangia ujenzi huu kwa no zifuatazo:-
Tigo – Pesa 0658 052 013, M – Pesa 0757 888 080 K.K.K.T MAGOMENI,
PICHA ZINAZOFUATA HAPA CHINI NI HATUA UJENZI ULIKOFIKIA MPAKA SASA.
Sehemu ya mbele ya kuingia katika kanisa jipya la Usharika wa K.K.K.T Magomeni Mviringo
Sehemu ya mbele inavyoonekana kwa sasa .Katikati unaweza kuona alama ya msalaba.Na mafundi wanaendelea na ujenzi
Ndani katika kanisa upande wa nyuma
Upande wa pembeni unavyoonekana kwa ndani
Upande wa nyuma nje ya kanisa unavyoonekana kwa sasa
Neno linaloongoza ibada hiyo ya harambee ya ujenzi linasema;
“Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa Mkamilifu; la!
WOTE MNAKARIBISHWA!
No comments: