Latest News


More

SOKA BRAZIL: UFARANSA YAFAIDI TECKNOLOJIA MPYA

Posted by : Unknown on : Monday, June 16, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :
Ufaransa yafaidi Teknolojia ya kuwasaidia marefarii Brazil 2014
Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufaidi matumizi ya teknolojia ya kisasa kuzuia ubishi katika mechi ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.
Karim Benzema alikuwa anatekeleza mashambulizi katika lango la Honduras kunaklo dakika ya 48 ya kipindi cha pili lakini kipa wa Honduras Noel Valladares akababaika na mpira ukavuka laini kisha akaunyofoa mara moja na
kukimbia akitaka kuupiga kama 'goal kick' lakini mpiga kipenga kutoka Brazil Sandro Meira Ricci akapuliza kipenga na kuashiria bao kutokana na mtikiso kwenye saa yake inayoambatana na teknolojia hiyo ya kisasa ya goal line.
Mashabiki na wachezaji wa Honduras waliokuwa ndani ya uwanja wa Porto Alegre walijaribu kupinga kauli ya refarii huyo lakini wapi alihakiki bao hilo la pili usiku huu kwa Ufaransa .
Honduras ilikuwa tayari imempoteza mchezaji wao Palacios mwisho wa kipindi cha kwanza alipoonyeshwa kadi ya pili ya manjano


Ufaransa yafaidi Teknolojia ya goaline dhidi ya Honduras Brazil 2014
Mfumo huo ambao tayari ushajaribiwa na Fifa, katika kombe la Mashirika mwaka uliopita.
Kampuni ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa, ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya michezo.
Hii itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa katika mfumo wa kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High Definition (UHD), ujulikanao kama 4K Format, ambayo kiwango chake ni mara nne zaidi ya kiwango chatelevisheni za kawaida.

Teknolojia hiyo inayotumika kwa mara ya kwanza inajumuisha kamera 14 za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa kurekodi picha na sauti kwa kasi mno na mpira ambao inasambaza
(Source:BBC Swahili)

No comments:

Leave a Reply