Mashindano ya Uimbaji wa Vijana ngazi ya Dayosisi
yamefanyika leo katika Usharika wa Mbezi Beach wa kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania na kushirikisha kwaya
za Vijana takriban toka sharika kumi na mbili za Dayosisi hii ya Mashariki na
Pwani
Katika mashindano hayo kwaya ya vijana ya Usharika wa Kimara (pichani juu)
imeibuka kidedea kwa kuchukua nafasi ya kwanza.Kwaya nyingine na nafasi zao ni
kamaifuatavyo
2.Nafasi ya pili imekwenda kwa kwaya ya Vijana ya Usharika
wa Ubongo
3. Nafasi ya tatu imekwenda kwa kwaya ya Vijana ya Usharika
wa Kijitonyama
4.Nafasi ya nne imechukuliwa na kwaya ya Vijana ya Usharika
wa Keko
5.Nafasi ya tano imekwenda kwa kwaya ya Vijana ya Usharika
wa Mwenge
Washindi wa pili kwaya ya Vijana ya Ubungo wakiimba jukwaani leo
Pichani juuna chini ni waimbaji wa kwaya ya Vijana ya Usharika wa Mwenge wakiimba jukwaani...Walishika nafasi ya tano
No comments: