Ufalme wa Mungu ni serikali halisi iliyoanzishwa na Yehova Mungu. Katika Biblia “
ufalme wa Mungu” pia huitwa “
ufalme wa mbinguni” kwa sababu unatawala kutoka mbinguni. (Marko 1:14, 15; Mathayo 4:17) Ufalme huo unafanana kwa njia fulani na serikali za wanadamu, lakini ufalme huo ni bora kuliko serikali hizo.
- Watawala. Mungu amemchagua Yesu Kristo kuwa Mfalme wa Ufalme huo na amempa mamlaka kuliko mtawala yeyote wa kibinadamu. (Mathayo 28:18) Yesu anatumia nguvu hizo vizuri, kwa kuwa tayari amethibitika kuwa Kiongozi mwenye kutegemeka na mwenye huruma. (Mathayo 4:23; Marko 1:40, 41; 6:31-34; Luka 7:11-17) Chini ya mwongozo wa Mungu, Yesu amechagua watu kutoka kwa mataifa yote ambao “
watatawala wakiwa wafalme
” pamoja naye huko mbinguni.—Ufunuo 5:9, 10. - Muda. Tofauti na serikali za wanadamu, ambazo hutawala kwa kipindi fulani na kisha kutoweka, Ufalme wa Mungu “
hautaharibiwa kamwe.
”—Danieli 2:44. - Raia. Mtu yeyote anayefanya mapenzi ya Mungu anaweza kuwa raia wa Ufalme wa Mungu, bila kujali ukoo au mahali alipozaliwa.—Matendo 10:34, 35.
- Sheria. Sheria (au amri) za Ufalme wa Mungu zinatimiza mambo mengi zaidi ya kukataza tabia mbaya. Zinasaidia raia wake kuwa wenye maadili mazuri. Kwa mfano, Biblia inasema: “‘
Lazima umpende Yehova Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili yako yote.’ Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza. Ya pili, kama hiyo, ni hii, ‘Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe.
’” (Mathayo 22:37-39) Kumpenda Mungu na jirani kunawachochea raia wa Ufalme huo wafanye mambo yanayowanufaisha wengine. - Elimu. Ingawa Ufalme wa Mungu unawawekea raia zake viwango vya juu, bado unawafundisha jinsi ya kutenda kulingana na viwango hivyo.—Isaya 48:17, 18.
- Lengo. Ufalme wa Mungu hauwafaidi watawala wake huku ukiwakandamiza raia wake. Badala yake utatimiza mapenzi ya Mungu kutia ndani ahadi ya kwamba wale wanaompenda wataishi milele katika dunia paradiso.—Isaya 35:1, 5, 6; Mathayo 6:10;Ufunuo 21:1-4.
No comments: