Latest News


More

MJUE MHUBIRI ALIYETEKA ROHO ZA WENGI NCHINI NIGERIA

Posted by : Unknown on : Friday, September 19, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :


Marais wengi Afrika wamemtembea Joshua wakitafuta kuombewa
Kanisa lililoporomoka mjini Lagos wiki jana , na kuwaua watu wengi, lilikuwa linamilikiwa na mhubiri anayesifika sana nchini Nigeria, TB Joshua.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anatufichulia haiba ya mhubiri huyu ambaye anadai amewaponya watu wakiwemo vipofu na waathiriwa wa HIV.
TB Joshua anadai kuwahi kutabiri matukio mengi kuanzia kwa kifo cha aliyekuwa gwiji wa muziki, Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia ya MH370"
Anajiita mtume na ni mmoja wa wahubiri mashuhuri sana nchini Nigeria ambako makanisa kama lake ni mengi kupindukia.
Alizaliwa mwaka 1963 tarehe 12 Juni katika familia maskini, akidai kwamba alikaa kwenye tumbo la mamake kwa miezi 15.
Baadaye katika maisha yake, anadai kuona kwenye ndoto yake manabii wakimtaka kuhubiri na kufanya miujiza.
Hapo ndipo alipoanzisha kanisa lake analoiita, 'Church of All Nations (SCOAN),' mwanzoni likiwa na waumini 8.
'Maji ya kuponya'
Wanaume na wanawake waanguka sakafuni wakati wakiombewa na TP Joshua
Hii leo Jushua kama wahubiri wengine nchini Nigeria, ni tajiri wa kupindukia akishabikiwa sana na watu nchini humo.
Watu huja kwake kutoka kote duniani wakitaka kuombewa wapone.
Wakati ugonjwa wa Ebola uliporipotiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, serikali ya jimbo la Lagos, ilimtambua muhubiri huyo kwa kuambia wagonjwa wa Ebola kwenda kwake akawaponye.
Alikubali kuahirisha baadhi ya programu za kanisa lake za kuponya lakini inaarifiwa alituma chupa 4,000 za maji ya ''uponyo' nchini Sierra Leone anayosema kuwa yanatibu magonjwa mengi tu.
TB Joshua anasema maji hayo ambayo yalitolewa kwa wagonjwa yakiwa ndani ya chupa ndogo, ndogo, yanaweza kuwasaidia wagonjwa kupona na kupata baraka.
'Utabiri'
Maelfu ya watu hutoka sehemu mbali mbali za dunia kutafuta kupona katika kanisa la TB Joshua
Anasifika, kwa unabii wake, TB Joshua anadai kutabiri matukio mbali mbali kuanzia kwa kifo cha marehemu Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia MH370.
Katika utabiri wake wa kifo cha Michael Jackson, TB Joshua aliwaambia waumini wake: ''Katika maeneo yake mwenyewe yeye ni mashuhuri. Najulikana kila sehemu. ''
''Kwa sababu mwanzo huwa naona kwamba kitu kitamfanyikia mtu flani mashuhuri, na kitu hicho kitamalizika, ila huwa sijui tu safari hiyo itakuwa lini. ''
Baada ya kifo cha Michael Jackson, mhubiri huyo alidai kuwa alikuwa amezungumzia kifo cha Jackson miezi sita kabla ya kutokea kwa kifo hicho.
Wakosoaji wake wanasema matamshi na utabiri wake ni wa kubahatisha.
Lakini hili halijawakoshesha usingizi waumini wa kanisa lake.
Joshua huandika vitabu na kutengeza kanda ambazo zinauzwa kupitia Internet
Mwanasiasa wa Afrika Kusini ,Julius Malema, Rais wa Malawi Joyce Banda, na mwanasiasa wa Zimbabwe,Morgan Tsvangirai na aliyekuwa Rais wa Ghana John Atta Mills, ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamemtembelea.
TB Joshua ni mmoja wa wahubiri mashuhuri barani Afrika.
Baadhi ya waumini wanadai kufaidika pakubwa kutokana na maombi yake, ni wale wanaosema wameweza kufanikiwa kifedha, kupona na hata watu kufufuliwa.
Nabii Joshua pia anajulikana kwa kazi yake kwa jamii ambayo yeye hujitolea.
Wengi nchini Nigeria hata huhofia kukmosoa TB Joshua.
(Source: BBC Swahili)

No comments:

Leave a Reply