Latest News


More

Apple kidedea katika faida zake

Posted by : Unknown on : Tuesday, February 3, 2015 0 comments
Unknown
Saved under :


Simu za Iphone 6 zimekuwa zikinunuliwa sana na kuwa chachu ya faida za kampuni ya Apple
Kampuni ya kutengeza vifaa vya elektroniki, Apple, imetangaza kupata faida ya dola bilioni 18.8 katika kipindi cha miezi minne ya mwisho mwaka jana , na kuifanya kuwa kampuni ya umma iliyopata faida kubwa zaidi duniani.

Apple bila shaka imeipiku,ExxonMobil iliyopata faida ya dola bilioni 15.9 mwaka 2012 kulingana na ripoti ya kampuni ya Standard and Poor's.
Inaarifiwa hii ndio faida kubwa zaidi katika historia ya kampuni hio kuwahi kushuhudiwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mdadaisi mkuu wa kiuchumi wa kampuni hio, Tim Cook alisema kuwa hitaji la simu za iphone duniani ni kubwa kuindukia.

Hata hivyo, alisema kwamba hitaji la tabiti au iPad haliko juu kama ilivyotarajiwa na liliendelea kushuka kwa asilimia 18 mwaka 2014 ikifananishwa na mwaka 2013.
Kadhalika hitaji la simu ya iPhone 6 Plus lilionekana kua chachu katika faida za kampuni hio.
Hata hivyo, Apple haikufafanua mauzo ya simu ya iPhone 6 na simu nyinginezo.
Hisa za kampuni ya Apple zilipanda kwa asilimia 5 baada ya soko la hisa Marekani kufungwa Jumanne.
Mmoja wa wanaofuatilia mauzo ya bidhaa za Apple sokoni, na mhariri wa mtandao wa "Cult of Mac" aliambia BBC kwamba mauzo ya iPhone yamekuwa juu sana ikilinganishwa na matarajio.

(Source:BBC Swahili)

No comments:

Leave a Reply