1 ELEWA JINSI MTOTO ANAVYOBADILI MAISHA YENU
- Baba: Msaidie mke wako kumtunza mtoto, hata kama ni usiku. Punguza muda unaotumia kufanya mambo mengine ili upate muda zaidi wa kuwa na mkeo pamoja na mtoto
- Mama: Mume wako anapojitolea kumtunza mtoto, kubali msaada wake. Ikiwa hafanyi vizuri, usimkosoe, badala yake kwa fadhili mwelekeze jinsi anavyopaswa kufanya
2 IMARISHENI UHUSIANO WENU
- Msisahau kupanga wakati wa kuwa pamoja peke yenu
- Usisahau kufanya mambo yatakayomwonyesha mwenzi wako kwamba unampenda, kama vile kumtumia ujumbe au kumnunulia zawadi
3 KUMZOEZA MTOTO WENU
- Mwombe Yehova akupe hekima ya kumfundisha mtoto wako
- Mtajie mtoto wako tena na tena maneno na mawazo makuu ili aanze kujifunza mapema
No comments: