Jumapili hii ilifanyoka ibada nzuri katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mtume Onesmo Ndegi (pichani juu) aliongoza na kuhubiri
Pichani juu Mtume Onesmo Ndegi akimtambulisha ndugu wa mke wake Lilian Ndegi ambapo pamoja na mambo mengine kulikua na uzinduzi wa Vitabu vya mwalimu Lilian Ndegi (ambaye ni mke wa Mtume ndegi)
Waumini wakifuatilia ibada hiyo jumapili katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe
Jumapili hii katika kanisa la Living Water Makuti Kawe ilifanyika ibada nzuri na ya baraka tele
Ibada hiyo ambayo pamoja na mambo mengine ilikua na mahafali ya wanafunzi wa Kozi ya Life Transforming iliongozwa na mkuu wa kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi akishirikiana na mwalimu Lilian Ndegi (pichani juu)
Waumini wakifuatilia ibada hiyo ya jumapili
Mwalimu Augustino akibubujika kwa maombi katika ibada hiyo
Apostle Onesmo Ndegi (mkuu wa kanisa la Living Water Center) akifurahi kwenye ibada hiyo.Kushoto kwake ni mwalimu Lilian Ndegi na watenda kazi wengine wa kanisa hilo
Apostle Ndegi akifurahi kwenye ibada hiyo ya jumapili
Mchungaji Naomi wa kanisa hilo akiimba kwa furaha
Pichani juu na chini ni waimbaji wa kwaya ya Living Water Center Makuti Kawe wakiimba kwenye ibada hiyo
Mpiga drums naye akiwajibika kwa sehemu yake
Waumini wakiimba na kucheza kwenye ibada hiyo ya jumapili
(Picha kwa hisani ya Gospel Kitaa Blog)
Posted on :
Thursday, March 26, 2015 [0] comments Label: Kutoka Madhabahuni
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha
Oviedo, nchini Hispania , wamegundua kwamba wanafunzi wanaofanya masomo
ya nyumbani ya sayansi na hisabati kwa zaidi ya dakika tisini hadi mia
moja ufanisi wao hushuka.
Nao Utafiti uliofanywa hivi karibuni na
wanasayansi umegundua kwamba masomo ya nyumbani apewayo mwanafunzi baada
ya saa za shule inashauriwa aifanye si zaidi ya dakika sitini sawa na
saa moja tu ili aifanye kwa ufanisi mkubwa.
Na endapo itamchukua
dakika tisini kuyafanya masomo hayo ya nyumbani matokeo yake hayatakuwa
mazuri, utafiti umebaini.utafiti mpya nao umeng’amua kwamba watoto
hawapaswi kusaidiwa na walezi ama wazazi wao kufanya masomo hayo ya
nyumbani.
Nao wanafunzi mar azote wamekuwa wakilalama kuwa masomo
ya nyumbani yakiwa mengi ni mbaya kwao, watafiti baada ya tafiti zao
wanakubaliana na malalmiko ya wanafunzi.
Kwa watoto walio katika
ukuaji na wanaojisomea kwa juhudi ili kupata matokeo mazuri,waalimu
hawapaswi kuandaa kazi ngumu kwa wanafunzi hao,lakini kazi ikiwa katika
daraja ya kati humfanya mwanafunzi kuelewa zaidi.
Dr Javier
Suarez-Alvarez anasema kwamba utafiti wao umeainisha kwamba hakuna
sababu ya mwalimu kumlimbikizia mazoezi mwanafunzi,lakini ni muhimu
mazoezi ya nyumbani yawe katika mpangilio ufaao kwa leo la kumfanya
mwanafunzi awe na mazoea ya kujifunza hata baada ya masomo ya darasani
na hii itamsaidia kupenda,uhuru na tabia ya kujisomea yeye binafsi hata
baada ya maisha ya shule .
JE UNATAMBUWA KUWA RUNDO LA KAZI ZA NYUMBANI HUMFANYA MWANAO AJIHISI MGONJWA? Utafiti wa hivi
karibuni,uliofanywa na chuo cha Stanford umegundua kuwa mwanafunzi
afanyapo masomo ya nyumbani kwa zaidi ya saa tatu kwa usiku mmoja
humfanya mwanafunzi augue.
Utafiti huo uliwahusisha wanafunzi elfu
nne na mia tatu kwa wanafunzi kumi bora wa shule za serikali hata za
binafsi katika jimbo la Califonia,na kuweka bayana kuwa masomo mengi ya
ziada humletea mwanafunzi msongo wa mawazo na kuleta matatizo mengine ya
kiafya.
Moja ya matatizo yanayotajwa ni msongo wa mawazo, lakini
pia masomo ya nyumbani yakiwa lukuki humletea mwanafunzi vidonda vya
tumbo,kukosa usingizi ama kupata usingizi wa mang’amung’amu,kupungua
uzito wa mwili ,na kuwa mchovu muda mwingi,huu ni utafiti alioufanya
Denise Pope. (Source:BBC Swahili)
Leo katika Usharika wa Mwenge wa kanisa la K.K.K.T imefanyika ibada ya familia ambayo imekua ya baraka kwa wote waliohudhuria
Katika ibada hiyo iliyopambwa na waimbaji wa kwaya ya Uinjilisti wa Usharika wa Sinza (pichani juu) pamoja na kwaya ya Umoja ya Usharika wa Mwenge
Ibada hiyo pia ilishuhudia ndoa mbili zikifungwa kwa pamoja na kisha kupata chakula cha pamoja hapo hapo Usharikani kwa waumini wote waliohudhuria ibada hiyo pamoja na maharusi na ndugu zao
Waimbaji wa kwaya ya Umoja wa Usharika wa Mwenge wakiimba ibadani jumapili hii
Mpigaji wa kinanda wa kwaya ya Uinjilisti Sinza akipapasa kinanda kwa ustadi mkubwa
Waimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Usharika wa Sinza wakiimba ibadani hapo
Mwimbaji kiongozi wa kwaya ya Uinjilisti Sinza akiongoza kipindi cha sifa.Nyuma yake ni waimbaji wa sifa wa Usharika wa Mwenge
Katika maisha ya siku hizi kuna changamoto nyingi zinazokabili familia mbalimbali
Akihubiri katika ibada ya jumapili ya leo katika Usharika wa Mwengemchungaji Ernest Kadiva wa kanisa la K.K.K.T amesema kuna changamoto nyingi zinazikabili familia zikiwepo;
1.Upendo kupoa pale ambapo na kipato kinapopungua
2.Teknolojia inachangia watoto kuharibika au kutotii mafundisho toka kwa wazazi na kanisa kwa ujumla
3.Familia kukosa nafasi ya kukaa pamoja (baba, mama na watoto) kutokana na mihangaiko ya kutafuta kipato hivyo kuchangia maadili ya watoto kuzidi kumomonyoka
Katika ibada hiyo kulikua na matendo mbalimbali yaliyofanyika kama vile kurudi kundini, ubatizo wa watoto wadodo, kipaimara kwa mkristo mmoja, shukrani za pekee, na ndoa mbili ambazo zimefungwa hivi leo Usharikani hapo na kisha kujumuika kwa chakula cha pamoja kwa washarika wote
Kwaya na vikundi mbalimbali vilijumuika kuimba ikiwepo kwaya ya Umoja ya Usharika wa Mwenge , kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza na mwimbaji binafsi mmoja
Kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza ikihudumu kwenye ibada hiyo jumapili ya leo
Waumini wakifuatilia ibada ya leo jumapili katika Usharika wa Mwenge
Katibu wa baraza la wazee wa Usharika wa Mwenge akifuatilia ibada hiyo.Pembeni ni mzee wa kanisa mama Seka Urio
Yesu Kristo akifundisha wanafunzi wake aliwaambia iweni wanyenyekevu kama walivyo watoto wadogo
Akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la .K.K.K.T Usharika wa mwinjilisti wa kujitegemea Godwin Gondwe alisema watoto wadogo huwa ni wanyenyekevu na hata kama wakiudhiwa huwa ni mara moja tu wanasahau na kufurahi
Bwana Godwin Gondwe ni mtangazaji wa kituo cha habari cha ITV na pia mkufunzi wa chuo kikuu cha Tumaini tawi la Dar es salaam
Ibada hiyo pia ilikua ya kusifu na kuabudu na ilihudhuriwa na vikundi vyote vya kwaya ya Usharika huo kama vile kwaya ya Uinjilisti, Kwaya kuu, kwaya ya Vijana, kwaya ya akina mama na pia mwimbaji wa kujitegemea Mwasabite
Liturjia iliongozwa na mchungaji kiongozi Mchungaji Kaanasia Msangi
Waumini mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo ya kusifu na kuabudu
Mwimbaji Mwasabiti akitunzwa na mzee Lema (mzee mstaafu wa kanisa hilo) wakati mwimbaji huyo akiimba wimbo wake wa Ni kwa neema na rehema
Mwimbaji Mwasabiti akiimba kwa hisani Usharikani Mwenge
Jana jumamosi katika Usharika wa Mbeze Beach wazee wastaafu na wapya wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani walifanya ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza salama vipindi vyao (kwa wale waliostaafu) na kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kuongoza watu wa Mungu kwa viongozi wapya
Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi takriban wote wa Dayosisi wakiongozwa na Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ambaye pia ni askofu wa dayosisi hiyo Dr Alex Gerhaz Malasusa.
Pamoja na viongozi wakuu wa Dayosisi pia walikuwepo baadhi ya wachungaji wa sharika mbalimbali na baadhi ya viongozi wa huduma ambazo ziko chini ya dayosisi hiyo kama vile Maendeleo Bank, Mtoni Diaconia Center, chuo kikuu cha Tumaini, Pendo Redio Nk
Pichani juu mkuu wa kanisa la K.K.K.T Askofu Dr Alex Malasusa akihubiri kwenye ibada hiyo
Baadhi ya wazee waliohudhuria ibada hiyo ya shukrani wakiwa kwenye ibada