Latest News


More

JUBILEE YA MWAKA YAFANYIKA MOSHI MJINI

Posted by : Unknown on : Friday, November 5, 2010 0 comments
Unknown
Saved under : ,

















Harusi ya nguvu ilifanyika mwishoni mwa mwezi wa kumi huko mjini Moshi kati ya Bwana na Bibi Rangia Mushi.Maharusi hawa walifanya Jubilee ya ndoa yao ya kutimiza miaka 50 tangu wafunge ndoa yao kwa mara ya kwanza.Ilikua harusi ya kufana na ilihudhuriwa na ndugu na marafiki wa karibu wa familia hii na ilifanyika katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Majengo mjini Moshi
Picha ya juu ikionyesha maharusi hao baada ya kutoka kanisani.
Hakika maharusi hawa walimeremeta sana
Ni jambo la kumshukuru sana Mungu kutimiza miaka 50 ndani ya ndoa.Shukrani za pekee ziwaendee watoto wa maharusi hawa ambao ndio waliofanikisha harusi na sherehe ya wanandoa hawa, wakiongozwa na Dr.Allen Mushi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam .Hakika mlifanya jambo la kukumbukwa na la baraka mbele za Mungu
Tunawatakia kila la heri maharusi hawa na Mungu awajalie maisha mema ya baraka tele
Amina!!








Maharusi wakiwa katika ukumbi wa sherehe.









Maharusi wakiwa tayari kupata picha ya kumbukumbu katika mzunguko wa kuelekea Arusha ambapo ni mahali maarufu sana kwa picha mjini Moshi









Picha juu maharusi baada ya kutoka kanisani wakiwa na watoto wapambaji wa harusi yao.Watoto hawa wadogo walikua ni wajukuu wa maharusi hao.


















Gari lililotumika kubeba maharusi.Hakika watoto wa maharusi hao walijiandaa sawa sawa kuwapamba wazazi wao na kuhakikisha wanatoka bomba.Hongera sana Dr.Allen Mushi kwa kazi nzuri










Maharusi wakiwa na wapambe wao baada ya kutoka kanisani








Maharusi wakiwa kwenye tabasamu la nguvu.
Hongereni sana Bwana na Bibi Rangia Mushi
Saved under : ,