Latest News


More

Wabunge watano machachari

Posted by : Unknown on : Thursday, November 4, 2010 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Wakati matokeo ya uchaguzi yakielekea ukingoni kutoka bunge lwa mwaka huu au la awamu hii linatua na sura mpya nyingi.Kati ya wabunge wateule ambao nadhani watatia chachu sana katika vikao vya bunge hapo Dodoma ni hawa wafuatao hapa chini
1.Halima Mdee wa Chadema
2.Mama Tibaijuka wa CCM
3.Bwana Mnyika wa Chadema
4.Mr Lyatonga Mrema wa TLP
5.Mr Mbilinyi (aka sugu) wa Chadema










Juu ni picha ya Halima Mdee wa Chadema mmojawapo wa mbunge kijana machachari wa Chadema.Huyu alikuwa kwenye bunge lililopita kama mwakilishi wa kuteuliwa.Lakini Mdee mwaka huu kaamua kusimama na kupigana na ameaonyesha hana sababu ya kusubiri viti vya kuteuliwa ila anaweza kusimama mwenyewe na kupambana hadi ushindi
I like it...Keep it up dada yangu





































Mama Tibaijuka.Huyu mama hakuna asiyemjua jinsi alivyokua anapambana na mambo ya makazi.Kipindi cha vurugu za uchaguzi huko Kenya alisimama kidete kuwatetea wale ambao walivunjiwa nyumba zao.Nadhani atakua na mchango mkubwa katika nchi yetu






































Bwana Mbilinyi aka sugu.Huyu ni mwanaharakati na mpiganaji halisi wa maswala ya unyanyasaji na kudai haki.Huyu bwana yuko radhi kuhatarisha usalama wake mradi tu apate haki yake.Wengi mtamkumbuka na album yake ya ant virus.Hii album inazungumzia haki za wasanii zinavyoibiwa.
Nadhani wasanii sasa mmepata mwakilishi wenu bungeni
Tunakutakia kila la heri










































Bwana Mnyika mmojawapo wa wabunge vijana wa bunge linalokuja.Kijana huyu naye ni mwanaharakati wa kutetea wanyonge na haswa vijana wasio na ajira.Nadhani naye ana mchango mkubwa sana katika bunge letu linalokuja
Kila la heri kaka






Bwana Lyatonga Mrema.Huyu hakuna asiye mjua katika nchi yetu.Amekua mmojawapo wa viongozi wa upinzania alieyeleta changamoto sana katika mageuzi hapa nchini.Amewahi kutumikia NCCR Mageuzi na sasa yuko TLP kama mbunge wa Vunjo.
Mchango wake bado tunaukumbuka akiwa waziri wa mambo ya ndani
Tunakutakia kila la heri baba