Latest News


More

Kijana amepotea

Posted by : Unknown on : Tuesday, July 19, 2011 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Kijana mwenye picha hapo juu amepotea
Kijana huyu alipotea maeneo ya Chang'ombe karibu na keko ambapo alikua anakaa kwa bibi yake Mama Sabina Lujuo kwenye nyumba zilizoko karibu na ofisi za TRA, Changombe karibu na Keko
Kijana huyu alikuja Dar toka Arusha kuja kwenye matibabu ambapo alikua anapata kwenye hospitali ya Muhimbili.Kijana huyu alikua ana tatizo kidogo la uelewa hivyo hata kuzungumza anazungumza kwa shida kidogo na hata uelewa wake ni mdogo pia
Kijana huyu alipotea wiki iliyopita ambapo alitoka nyumbani kama anatembea kidogo na hakurudi tena mpaka leo hii

Taarifa zimetolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hata polisi bila mafanikio

Wajihi wake
Anaitwa - Edward Stevin
Jinsia - Mwanaume
Rangi - Ni mweusi, mrefu kidogo
Umri - kati ya miaka 21 na 22
Nguo alizofaa - Suruali ya jeans blue, T.shirt ya Blue (yenye maandishi Thunder crazy)
Viatu - raba nyeusi (za reebok)
Alama - ana alama kwenye paji la uso (kovu dogo jeusi) kwenye shavu la kushoto

Yeyote atakayemwona tunaomba atoe taarifa kituo chochote cha polisi
Au apige simu zifuatazo
0754-270952, 0715- 270952