Latest News


More

Honeymoon yageuka na kusababisha kifo

Posted by : Unknown on : Wednesday, August 17, 2011 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Raia mmoja wa Uingereza ameuawa na samaki aina ya Shark alipokua anaogelea pembezoni mwa beach moja wakati wa honeymoon huko katika visiwa vya Sychelles
Raia huyo Ian Redmond ameuawa wakati akiogelea katika beach maarufu ya Anse Lazio katika kisiwa kidogo cha Praslin
Inaaminika kuwa raia huyo (miaka 30) aliefunga ndoa karibu wiki mbili zilizopita alikuwaakiogelea kwenye kina cha maji maji marefu ambapo mkewe mwenye miaka 27 Gemma Houghton alikua amekaa yadi kama 20 toka alikokua akiogelea bwana huyo
Bwana huyo alikamatwa na samaki huyo aina ya shark na alimvunja mkono mmoja , mguu na kumrarua vibaya sehemu ya kifua
Jeanne Vargiolu, mwenye miaka 56 na mmiliki wa mgahawa wa Le Chevalier kwenye beach hiyo alisema mke wa marehemu huyo alikua ana matumaini ya kupona mumewe wakati mumewe alipokua amelala mchangani hajiwezi
Lakini polisi walipofika walisema hakukua na matumaini ya kupona kwa raia huyo wa Uingereza kutokana na majeraha makubwa aliyopata.
Saved under : ,