Latest News


More

Posted by : Unknown on : Monday, August 22, 2011 0 comments
Unknown
Saved under : ,
KIJANA ALIYEPOTEA AMEPATIKANA


Kijana aliyeripotiwa kupotea takriban wiki tatu sasa amepatikana
Kijana huyo pichani juu alipatikana huko Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.Kwa mujibu wa maelezo yake kijana huyo ambaye ana tatizo kidogo la akili alisema baada ya kutoka nyumbani alikokua anaishi na bibi yake (huko Chang'ombe Bora) , alishindwa kujua njia ya kurudi nyumbani hivyo akawa anaendelea kwenda asipopajua mkapa alivyotokea huko Vikindu.
Kijana huyo aliletwa na mama msamaria mwema baada ya kumwomba akirandaranda maeneo ya nyumba yake huko Vikindu
Kwa mujibu wa maelezo yake kijana huyo baada ya kupotea alikua analala barazani kwa watu na wakati mwingine kwenye nyumba au vibanda vibovu.Kula kwake nako kulikua ni kwa kuomba omba na wakati mwingine alikua anashinda na kulala na njaa


Picha ya kijana huyo aliyopiga siku aliporudi nyumnbani kwa bibi yake Sabina Lujuo


Kama familia tunapenda kuwashukuru wale wote waliotuombea na kutupa moyo kwa kipindi chote hiki, vyombo vya habari kama televisheni, radio na blogs ambazo zilitoa tangazo la kupotea kijana wetu huyu na hata kuweza kupatikana na kurudi tena nyumbani
Mungu awabariki sana, sisi kama familia hatuna cha kuwalipa ila Mungu mpaji wa yote ndiye atakayewalipa
Ahsanteni
Mama Sabina Lujuo
(kwa niaba ya familia)