Latest News


More

BARAKA TOKA KWA MUNGU

Posted by : Unknown on : Tuesday, April 9, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,


Bwana Yesu asifiwe wapendwa wana blog ya tumani letu (iliyokuwa inaitwa kichila.blogspot.com) Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu alitupa mimi na wewe neema na baraka ya kuona tena siku hii ya leo.Nasema ni neema kwani ni wengi wetu walitamani lakini wameshindwa, wengine wako hospitalini au majumbani wamelala wanaumwa lakini wengine wamekwishakata roho hawako tena katika ulimwengu huu.Mimi na wewe ni nani hata tuwe na afya njema ? Hayamkini Mungu ana makusudi maalum na mimi na wewe tuliye na afya njema leo.

Ni takriban miaka mitatu tangu nianzishe hii blog kwa ajili ya kupeana habari mbalimbali ikiwa na jina kichila.blogspot.com Ni wiki moja sasa imepita mtaona kuna mabadiliko ya jina na kuwa tumainiletu.blogspot.com.Hii ni baada ya kupata ushauri toka kwa mtaalam wa mambo ya blog (bwana Makule) baada ya kumweleza nia na madhumuni yangu ya kujikita zaidi katika injili na muziki wa injili kwa ujumla wake. Hivyo jina pamoja na mmwonekano mzima mtaona umeboroshwa zaidi ili kuifanya kuwa ya kisasa zaidi Hivyo bado tunaendelea kuifanyia ukarabati hadi hapo itakapoonekana imekua nzuri zaidi na zaidi.

Nakaribisha maoni, ushauri wa jinsi ya kuifanya bora zaidi. Nia ni kutaka itumike kwa mambo ya kupeleka injili sehemu mbalimbali duniani pamoja na nyimbo za injili kwa ujumla wake Pia nikaribishe wote ambao wanataka kutuma masomo au mafundisho yao katika blog hii, au kama kuna anayetaka kutangaza huduma yake anakaribishwa kwa mikono miwili kwa sasa wakati tuko kwenye kipindi cha mpito.Pia kama kuna semina, uzinduzi wa nyimbo za injili, mikutano ya injili n.k

Mnaweza kuwasiliana nasi kwa anwani ifuatayo;
Anwani ya Barua pepe:kichilat@gmail.com au kichila_ts@yahoo.co.uk
Simu: 0655-111342 au 0757-111343

Mungu awabariki na nawatakia kila la heri katika kumtumikia Mungu wetu aliye hai YESU KRISTO Mbarikiwe!!! TUMAINI KICHILA...(Founder. tumainiletu.blogspot.com)

(Mshukuruni Bwana kwa kuiwa ni mwema;kwa maana fadhili zake ni za milele....Zab 136:1)

No comments:

Leave a Reply