Latest News


More

MWIMBAJI WA KWAYA YA VIJANA ATANGAZA NIA

Posted by : Unknown on : Saturday, May 25, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Mwimbaji wa kwaya ya Vijana na kwaya kuu ya Usharika wa K.K.K.T Usharika wa Mwenge ndugu Isaya Mhema jumapili iliyopita alitangaza nia ya kumwoa bi Christina.Bwana Isaya alitangaza nia hiyo katika ibada iliyofanyika kanisani hapo , ibada ambayo iliongozwa na Mchungaji kiongozi wa Usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi
Katika ibada hiyo iliyokuwa ni ibada ya kusifu na kuabudu mwimbaji huyo alimvisha pete ya uchumba bi Christina tendo ambalo liliongozwa na mchungaji wa Usharika
Pichani juu Bwana Isaya akiwa na bi Christine mara baada ya kumvisha pete ya uchumba
 Bwana Isaya baada ya kumtambua mchumba wake anampeleka mbele ya Usharika tayari kumtambulisha.Nyuma ni wanakwaya wenzake wakimshangilia
 Mchungaji Kaanasia Msangi akizungumza machache kabla ya kufanya sala.
 Mchungaji kiongozi Mchungaji Kaanasia Msangi fanya sala na Bwana Isaya na Bi Christina
 Wanakwaya ya kwaya ya Uinjilisti wakiimba kwenye ibada hiyo

Waimbaji wa kwaya ya Vijana na kwaya ya Uinjilisti wakimpongeza Bwana Isaya na Bi Christina
Wanakwaya wa kwaya ya Uinjilisti wakiimba kwa furaha kwenye ibada hiyo
Tunawatakia kila la heri wachumba hawa katika maandalizi yao ya kuwa mwili mmoja

No comments:

Leave a Reply