Latest News


More

DUNIA INAELEKEA WAPI?MUASI AULA MOYO WA MWANAJESHI ALIYEUAWA - SYRIA

Posted by : Unknown on : Saturday, May 25, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,
 Wapendwa ebu sikieni hiki kisa !

Kisa cha hivi karibuni cha Muasi nchini Syria kuula moyo wa mwanajeshi aliyeuawa, kiliwashangaza wengi. Lakini tukio kama hili je ndilo la kinyama zaidi kuliko matukio mengi yanayoshuhudiwa katika maeneo ya vita?
Tumezoea kusikia ripoti za makaburi ya halaiki, vyumba vya mateso, mauaji na kukatwa katwa miili ya watu na hata kuwaangamiza watu katika kijiji kizima.
Lakini kitendo hiki cha kula moyo wa adui, bila shaka kimezua hisia kali. Binadamu kumla mwenziwe ni jambo linalokiuka maadili na hata baadhi ya imani za watu kuhusu kinachoweza kutendeka katika katika maeneo ya vita.
Kwa hivyo je ghasia za Syria zimefika kiwango gani na je ni dalili gani za kuonyesha ikiwango hicho?
Je ni nini kinachosababisha watu katika maeneo ya vita kufika kiwango hiki cha kula wengine?
Katika mahojiano na wapiganaji 2,500 wa zamani kutoka Uganda, Rwanda, Colombia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
iligunduliwa kuwa vitendo vinavyofanyika katika maeneo hayo sio vichache ukilinganisha na kile kichotokea nchini Syria.
Kinyume na hilo, wakati maadili ya kijamii yanapoporomoka huku ghasia zikianza kutokea ishara ya vita, basi maadili yanayolinda binadamu kutokana na binadamu mwenzake nayo yanapotoka.
HAKIKA WATU WA MUNGU TUNAHITAJI MAOMBI ZAIDI ILI MUNGU ATUKOMBOE KUTOKA KWENYE MKONO WA SHETANI!!
(Picha kwa hisani ya bbcswahili.com)

No comments:

Leave a Reply